Menu
NDOTO ZANGU
  • Home
  • Orodha ya Ndoto
  • Quizzes & Surveys
  • Contant
  • English Articles
  • Kuhusu
  • MASOMO KWA WANAWAKE
NDOTO ZANGU

SITIRI MWILI WAKO, USIWE CHANZO CHA MWENGINE KUTAMANI

Posted on October 30, 2022October 30, 2022

FUNDISHO MAALUMU KWA MWANAMKE

Jina la Bwana na Mungu Wetu Yesu Kristo litukuzwe daima, ikiwa wewe ni dada, binti, au mama, basi nakukaribisha tujifunze neno la Mungu kwa pamoja.

Kama mwanamke, unapaswa uwe nadhifu kwa kuusitiri mwili wako pale uwapo sehemu za mkusanyiko wa watu wengi hasa wa jinsia tofauti (hasa kwa wale walio dhaifu rohoni), ili usiwe chanzo cha wao kutamani na kuzini nawe mioyoni mwao, kwa sababu asili ya mwili wa mwamke endapo hautokuwa umesitiliwa vizuri ni kutamanika na kuinua vishawishi.

Kumbukumbu La Torati 5:21 WALA USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala kitu cho chote alicho nacho jirani yako.

Umeona hapo? Biblia inaposema usimtamani mke wa jirani yako, maana yake ni kuwa, asili ya mwanamke siku zote  ni kutamanika, na asili hiyo inaweza mwangumsha mtu yoyote yule katika dhambi hata kama anatembea na Mungu kiasi gani (endapo tu, asipotaka kuisukumia mbali na kuwa makini kama mfalme Daudi alivyoanguka pale alipomtazama mke wa askari wake uria na kumtamani), Hiyo ni mbaya sana.

Na tena hata tukisoma katika (Mathayo 5:28) maandiko yanasema..

Matayo 5:28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu AMTAZAMAYE MWANAMKE KWA KUMTAMANI, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Lakini pia, hata ukisoma (Ayubu 31:1), (2 Samweli 11:2), (Kutoka 20:17), (Ezekiel 22:11), Vina toa picha ile ile kuwa, sifa moja wapo ya mwanamke ni kutamanika,  na ni dhambi inayoweza mpeleka mtu jehanam kabisa kwa kumtaza na kumtamani tu mwamke, na ndio maana, kwa kuliepusha hilo katika kanisa, mtume Paulo kwa kuongozwa na Roho wa Bwana, aliandika hivi kwa wanawake wote wa wakristo duniani wanao ukiri uchaji wa Mungu.

1 Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe KWA MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;

Ikiwa na maana kwamba, endapo katika kanisa, wanawake wasipo vaa mavazi yanayositiri miili yao, inaweza pelekea ushawishi mkubwa sana wa dhambi ya uzinzi na usharati katika kanisa.

Mama/binti (uliyeokoka na usiyeokoka), usipousitiri mwili wako kwa mavazi ya adili na heshima, tambua kwamba, unakuwa sababu kubwa ya kuwakosesha watu ambao ni dhaifu rohoni na kuwafanya wakutamani na kuzini na wewe mioyoni mwao, unapovaa nguo inayonesha mapaja yako, unawafanya wanaokutazama na kukutamani wanazini na wewe mioyoni mwao, unapovaa nguo inayoonesha mgongo wako, maziwa yako, tumbo lako, kitovu chako, unawafanya wanaokutazama na kukutamani wazini na wewe mioyoni mwao, unapovaa suruali inayochora makalio yako na maungo yako ya sehemu zako za siri, unawafanya wanaokutazama na kukutamani wanazini na wewe mioyoni mwao, na tena, unaweza pelekea hata wanaume walio dhaifu zaidi kwenda kufanya musterbration (kujichua) kwa ajili yako, hivyo, unaweza jikuta kwa siku umezini na watu zaidi hata themanini (80) mioyoni mwao kwa kukutamani tu! Je! Unalitambua hilo?

Sasa jiulize, endapo nafsi hizo zote zilizokutamani na kuzini nawe mioyoni mwao zikifa bila kutubu zitaenda wapi kama si kuzimu? Na je! Bwana atakuachia wewe uliyesababisha nafsi hizo kupotea? Jibu ni hapana, Bwana hatokuachia na wewe (endapo usipotaka kutubu na kubadirika), kwani imeandikwa..

Marko 9:42 NA YE YOTE ATAKAYEMKOSESHA MMOJAWAPO WA WADOGO HAWA WAAMINIO, AFADHALI AFUNGIWE JIWE LA KUSAGIA SHINGONI MWAKE, NA KUTUPWA BAHARINI.

Hivyo basi, Sitiri sasa mwili wako mwanamke ili usiwe chanzo cha mwengine kukutamani, haijalishi uliwakosesha wangapi, haijalishi ulitembea nusu uchi barabarani mara ngapi, haijalishi ulivaa nusu uchi night clubs mara ngapi, haijalishi ulivaa nusu uchi kwenye bar mara ngapi, unachotakiwa kufanya ni kuacha, kutubu kwa kumwamini Yesu Kristo na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, nawe utapokea kipawa cha Roho Mtakatifu, atakaye kubadilisha na kukufanya kuwa mwamke mpya kabisa.

Tafadhari, washirikishe na wanawake wengine ujumbe huu;

Bwana akubariki, Shalom.

Mada zinginezo:

Mtupe chini Yezebeli kama unataka kuwa upande wa Mungu

Nini maana ya huu mstari huu HUWEKA NYUMBANI MWANAMKE ALIYE TASA, AWE MAMA YA WATOTO MWENYE FURAHA

JINA LAKO LIMEANDIKWA KATIKA KITABU CHA UZIMA?

MASOMO KWA WANAWAKE

4 thoughts on “SITIRI MWILI WAKO, USIWE CHANZO CHA MWENGINE KUTAMANI”

  1. Prisca komba says:
    November 26, 2022 at 1:48 pm

    Amina Kumwa

    Reply
    1. Magdalena says:
      December 6, 2022 at 10:17 am

      Amen dada

      Reply
    2. watakatifuwasikuzamwisho says:
      December 19, 2022 at 1:22 pm

      Amen

      Reply
  2. Goodluck says:
    December 28, 2022 at 6:48 pm

    Amina

    Reply

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts

  • BWANA AKALIZIDISHA KANISA KWA WALE WALIOKUWA WAKIOKOLEWA
  • TAFAKARI KWAKO MKRISTO.
  • ZIWA LA MOTO
  • TOKA KWA VIONGOZI VIPOFU.
  • KUOTA UMEKUFA

Recent Comments

  1. Magdalena on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  2. Goodluck on SITIRI MWILI WAKO, USIWE CHANZO CHA MWENGINE KUTAMANI
  3. Goodluck on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  4. Magdalena on USIMNAJISI BINTI YAKO, ILI KUMFANYA AWE KAHABA.
  5. watakatifuwasikuzamwisho on Je! Ni wanawake gani wanazungumziwa katika (Zaburi 68:11)?

Archives

  • January 2023
  • December 2022
  • November 2022
  • October 2022
  • September 2022
  • August 2022
  • June 2022
  • May 2022
  • April 2022
  • March 2022
  • February 2022
  • December 2021
  • November 2021

Categories

  • Ndoto kutoka kwa Mungu.
  • Ndoto za Adui (shetani)
  • Ndoto za tahadhari.
  • Uncategorized
  • Wanawake

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2023 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress