Embu tulisome hilo andiko….
Zaburi 113:4-9
[4]BWANA ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu.[5]Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
[6]Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?[7]Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.[8]Amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake.[9]Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa,
Awe mama ya watoto mwenye furaha.
JIBU..
Ukisoma kuanzia juu utaona mwandishi anajaribu kueleza ukuu na uweza wa Mungu jinsi ulivyo wa ajabu..Jinsi gani kwake Bwana hakuna majira wala nyakati,hana kuchelewa wala kuwahi..ukuu wake ni mkuu zaidi….
Kwa mwandamu namna hii haiwezi kuonekana kwa ukamilifu wowote…mwanadamu majira ya mvua yakipita kwake basi anaamini mvua haitanyesha mpaka yale majira yarudi tena kwa msimu mwingine..mwanadamu akikosa chakula leo anaamini ndo kashalala njaa hivyo…mwanadamu akipungukiwa chochote anajiwekea imani kuwa hataweza kukipata tena…ndo mana ukisoma kuanzia juu anasema….
Zaburi 113:5
[5]Ni nani aliye mfano wa BWANA,
Mungu wetu aketiye juu;
Hakuna aliye na Mfano kama Mungu wetu,ambaye kwake majira,nyakati,msimu au lolote linaweza kumfanya asifanye kama atakavyo…humwinua yeye aliyedharaulika na kuonekana kama kinyesi akamtukuza na kumsimamisha kwa ukuu wake!! yeye hufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyafanya wala kuyafikiri kwamba yanawezekana….
Na ndo mana huo mstari wa tisa anahitimisha kwa kusema,HUMWEKA NYUMBANI MWANAMKE ALIYE TASA AWE MAMA YA WATOTO WENGI…
akimaanisha,humfanya mwanamke asiye weza kuzaa akaolewa na utasa wake na kumfanya awe mama wa watoto wengi,(mwanamke aliyeolewa ni sawa la aliyewekwa nyumbani na mumewe)
Jambo hili kwa mwandamu ni kubwa sana…lakini kwa Bwana linawezekana….
Mama,Mwanamke..umekuwa ukiteseka kwa muda mwingi ukihangaika huku na huko ili upate uzao lakini imeshindikana…kwenye ndoa yako imepita miaka mingi pasipo kuona dalili zozote za ujauzito mpaka umeona ndoa ni chungu….ni kweli madaktari wanasema huna uwezo wa kushika mimba kwasababu kizazi kimeharibika au hakipo…umeona heri ukate tamaa ya kuendelea na ndoa yako kutokana na masimango na manyanyaso unayopitia….
Kweli kwako imeshindikana lakini sio KWA YESU KRISTO!!!!yeye anasema humweka nyumbani mwanamke aliye tasa,awe mama ya watoto mwenye furaha…Mkimbilie daktari mkuu akuponye udhaifu wako,Yesu ndiye awezaye kufungua tumbo lako,Yesu Kristo ndiye mwenye uwezo wa kukupa furaha ya kuwa na watoto,Yesu pekee ndiye MSAADA mkuu wa wakati wote…
Hali unayopitia wewe sio wa kwanza,embu mkumbuke mwanamke Sara na Hana,jinsi Bwana alivyowatendea mambo makubwa na ya ajabu!!mpaka Sara anajiuliza…
Mwanzo 21:7
[7]Akasema, N’nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
Mungu hajawahi kushindwa kwa kitu chochote kile…
Maandiko yanasema….
Isaya 54:1
[1]Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA.
Mkimbilie Bwana awezaye kubadili mambo yote kama apendavyo kwa utukufu wa jina lake…lakini kama uko nje ya wokovu mambo hayo utayasikia tu kwa wengine wakitendewa miujiza hiyo….Sharti kama ujaokoka ni lazima umkabidhi yeye maisha yako kwa kumkiri kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako na kisha utubu dhambi zako zote na baada ya hapo Ukabatizwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina lake YESU KRISTO…
Baada ya hapo utakuwa milki halali ya Mungu,na utaanza kuona mambo makubwa na ya ajabu Mungu atakayokutendea..
Usichelewe saa ya wokovu ndiyo sasa,sio badae wala kesho…
Shalom…Wasambazie na wengine habari hizi njema kwa kushea..
Bwana wetu anakuja…..