Blogu hii ni kwa lengo la kusaidia kupata au kujua tafsiri za ndoto mbali mbali tunazoziota kila siku.
Tafsiri za ndoto zote ndani ya tovuti hii zimetafsiriwa au kugawanywa kulingana na kitabu kimoja tu! Ambacho ni “BIBLIA TAKATIFU” Na wala si kitabu kingine chochote cha Sayansi wala cha Dini nyingine yoyote isiyotumia Biblia.
kiini cha Imani ni YESU KRISTO. Tunaamini Yesu Kristo, ndiye Njia, Kweli na Uzima. Wokovu unapatikana kwake Mwenyewe na wala si mwingine yeyote, na alikufa, akafufuka, akapaa mbinguni na atarudi tena kwa hukumu ya Mwisho. Na kila amwaminiye na kubatizwa ataokoka (Marko 16:16).