FUNDISHO MAALUMU KWA MWANAMKE
Shalom, Jina la Mwokozi Wetu Yesu Kristo litukuzwe milele na milele, sifa na ukuu ni vyake. Amina, karibu tujifunze neno la Mungu.
Kama wewe ni mwanamke (mama au binti), unayetaka kumcha Mungu na kuwa upande wake daima kama ilivyokuwa kwa wanawake walioutii uchaji wa Mungu kama Sara, Hana, Mariamu, Elizabeth, n.k, basi huna budi kwanza KUMTUPA CHINI YEZEBELI.
Ili tuelewe vizuri, tusome kwanza habari ifuatayo katika maandiko matakatifu (ZINGATIA MANENO YALIYOANDIKWA KWA HERUFI KUBWA)
2 Wafalme 9:30 Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; AKATIA UWANJA MACHONI MWAKE, AKAPAMBA KICHWA CHAKE, akachungulia dirishani.
31 Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako?
32 Akainua uso wake kulielekea dirisha, AKASEMA, ALIYE UPANDE WANGU NI NANI? Matowashi wawili watatu wakachungulia.
33 AKASEMA, MTUPENI CHINI. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga.
Katika habari hiyo, Yehu aliyekuwa ni mmoja wa majemedari wa jeshi la Taifa la Israeli, mtiwa mafuta wa Bwana. Sasa tunasoma katika habari hiyo kuwa, Yehu aliuliza “ALIYE UPANDE WANGU NI NANI?” Ikimaanisha kwamba, endapo ungekuwa upande wa Yehu, basi ungekuwa upande wa Bwana, kwa sababu Bwana Mwenyewe alimchangua Yehu mwana wa Nimshi kuwa mfale juu ya watu wa Israeli, na pia kwa lengo la kulipiza kisasi chake kwa ajili ya watumishi wake manabii katika nyumba ya Ahabu na Yerebeli (2 Mambo ya Nyakati 9:7),
Baada ya Yehu kuuliza lile swali tunasoma matowashi wawili watatu walichungulia dirishani kuashiria kuwa, wapo tayari na wanataka kuwa upande wa Yehu ambao ndio upande wa Bwana, na baada ya kuonesha nia hiyo Yehu aliwaambia wamtupe chini kwanza mwanamke Yezebeli na walifanya hivyo.
HII INAFUNUA NINI SASA KATIKA ROHO?
Towashi ni mtu aliyehasiwa au aliyeamua kutoa maisha yake binafsi kwa ajili ya kumtumikia bwana wake tu! Na mfano wa towashi ni yule mkushi aliyekutana na Filipo mhubiri wa injili wanakati anatoka Yerusalemu kuabudu (Matendo 8:27), na sisi pia katika roho hatuna budi kuasiwa kwa habari ya mambo ya udunia ili tumpendeze Bwana Wetu Yesu na tuishi kwa ajikibyake tu! Hallelujah…
Na swali lile lile hata sasa pia Mungu anawauliza wanawake wote matowashi rohoni, walioasiwa kwa habari ya udunia na tamaa zake lakini bado hawapo upande wa Yehu (upande wa Bwana), ALIYE UPANDE WANGU NI NANI? Anawauliza wanawake wote waliopo chini ya jua wanaotaka kuwa upande wake, anawauliza bila kujali rangi, umri, cheo, wala elimu, na Kama upo tayari kuwa upande wa Bwana leo hii, basi huna budi kwanza KUMTUPA CHINI HUYO YEZEBELI wewe mwanamke towashi rohoni,
Na Yezebeli wa kumtupa chini sio Yezebeli wa kimwili bali wa rohoni, ambaye matendo yake na roho yake kama hayo ya kujipaka wanja na kuipodoa yanafanya kazi hadi sasa ulimwenguni (matendo hayo ndiyo Yezebeli mwenyewe unayepaswa kumtupa chini kama unataka kuwa upande wa Bwana), tupa chini kupaka wanja mwanamke na make-up, lipstick na kujichubua ngozi yako, kuweza mawigi kichwani na nywele bandia, kucha bandia, kope bandia, kutia dawa nywele zako za asili ulizopewa na Mungu, kuvaa hereni, mikufu, na mabangiri, kuvaa nguo zinazoonesha na kuchora maungo yako mwanamke, kuvaa suruali, nusu uchi, vimini, nguo zinazoonesha sehemu za ndani za mwili wako kama mapaja, tumbo, maziwa yako, mgongo wako na kitovu chako, na matendo yote machafu yanayofanana na hayo juu ya mwili wako, huyo ndiye Yezebeli unayepaswa kumtupa chini kama kweli unataka kuwa upande wa Bwana.
Kumbuka: kwa nguvu zako hutoweza kama uko nje Wokovu, sasa ili uweze kumtupa chini Yezebeli sharti ni ukubali kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako na utubu dhambi zako zote kwa moyo wako na kisha ukabatizwe ubatizo sahihi ili Yesu akupe nguvu na u mtupe chini Yezebeli (kuyatupa chini matendo yote mabaya)
Mtupe chini Yezebeli wa matendo yote maovu, Yasiyompendeza Bwana
Tafadhari, washirikishe na wanawake wengine ujumbe huu;
Bwana akubariki, Shalom.
Mada nyinginezo:
Nini maana ya huu mstari HUWEKA NYUMBANI MWANAMKE ALIYE TASA, AWE MAMA YA WATOTO MWENYE FURAHA
Ubarikiwe dada
Amina barikiwa… pia zidi kujifunza zaidi
Na ukiwa na swali lolote ambalo utahitaji kujifunza zaidi kuhusu biblia karibu