Nakusalimu Kwa Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo, Karibu tujifunze Neno la Mungu ambalo ndio taa na mwanga wa maisha yetu….
Leo kwa Neema za Bwana tutajifunza mambo kutoka kwa wanawake watakatifu wa zamani, naamini wewe kama Binti, dada,Mama, una cha kujifunza kutoka kwa hawa wanawake
Lakini kabla ya kuendelea mbele hebu tueke msingi kidogo,…. maisha yetu sisi wanadamu yana nafasi tofauti tofauti kulinganana na mazingira,na kuna sehemu unafika unaona kuna vitu naweza kuvimudu mwenyewe kwa akili zangu na kuna vingine unaona kabisa hapa nahitaji kujifunza kwa mtu,au kitu fulani,
Kwa mfano tuchukulie ni mtu anayetaka kufanya biashara,ana mtaji wa kutosha ana idea nyingi za biashara tofauti tofauti, ana mipango mingi ya biashara kubwa za kufanya kulingana na mtaji wake lakini asipotaka mashauri kutoka wa wafanyabiashara waliomtangulia na kujifunza kwao, uwezekano wa yeye kufilisika kwenye biashara yoyote atakayoianzisha ni rahisi sana kama hatataka kujifunza kwa wengine…..
Hata sasa kwa watakatifu wote duniani, Maandiko Matakatifu ndio mtaji wetu sisi,ina maana mshauri yote, mipango yote ya kuwekeza katika ufalme wa Mungu ipo katika Biblia takatifu kama hatutataka kujifunza na kuchukua mashauri yake,tutafeli tu……
Maandiko yanasema,…
1 Petro 3:5
[5]Maana hivyo ndivyo walivyojipamba WANAWAKE WATAKATIFU WA ZAMANI,WALIOMTUMAINI MUNGU na kuwatii waume zao.
zingatia maneno yaliyoandikwa kwa herufi kubwa,,,
Embu tuwatazame kwa ufupi baadhi kwa ya hawa wanawake na sisi tupate la kujifunza…..
SARA”
Nadhani wote tumeshalisikia hili jina mpka limekuwa desturi kwetu, lakini leo hatutangia ndani zaidi,Kama tunavyomfahamu ni mwanamke ambaye aliamua kusimama kwenye nafasi yake ya Usaidizi kwenye familia yake mpka kwa muwewe Ibrahimu,
Alijua kabisa yeye ndo mwanamke,akiwa mpumbavu ataivunja ndoa yake,akijitoa ufahamu basi atayumbishwa na mambo ya ulimwengu hu,akajua lipo jambo moja tu litakaloweza kufanya mambo yote ni KUMTUMAINI MUNGU,mpaka anafikia muda anabadilishwa jina hakuwa mwanamke wa leo hapa kesho kule,alijua zipo Baraka kwa wale wanaomtumainia Bwana… ndipo hapo tunaona hata Katika uzee wake Mungu anambariki kwa mtoto jambo ambalo lilikuwa haliwezekaniki….
Mwanzo 21:6-7
[6]Sara akasema, Mungu amenifanyia kicheko; kila asikiaye atacheka pamoja nami.
[7]Akasema, N’nani angemwambia Ibrahimu, Sara atanyonyesha wana? Maana nimemzalia mwana katika uzee wake.
HANA”
Tunapomsoma Hana au mtoto wake aitwae Samweli tusidhanie ilikuwa ni habari tu iliyoandikwa ili itufurahishe,lipo jambo ambalo tukilisoma kwa umakini tutajifunza mambo mengi sana,
Hana alikuwa ni mwanamke aliyepitia mateso ya manyanyaso sana, kila kukicha kwake ilikuwa ni kama giza, tena alikuwa ni mke mwenza kama ulikuwa hufahamu….
1 Samweli 1:1-2
[1]Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu
[2]naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto.
Umeona hapo,nadhani kila mmoja anajua shida iliyopo kwenye maisha ya wake wenza,ni mara chache sana uwakute wanaishi kwa amani,tena tunaona Hana hakuwa na mtoto kwsababu Mungu alimfunga tumbo,, ni jinsi gani kilivokuwa kipindi kigumu sana kwa mwanamke huyu,
Lakini tunaona pamoja na hayo yote,hana hakukata tamaa,hakurudi nyuma ijapokuwa muwewe alimpenda,alijua yupo mmoja tu aliye tumaini lake ambaye hata dunia imtenge, ndugu wamkane,ulimwengu umcheke, bado hataacha kumtumainia Mungu,.
1 Samweli 1:,13,15-17
[13]Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
[15]Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA.
[16]Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.
[17]Ndipo Eli akajibu, akasema, Enenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.
NABII ANA”
Huyu ni mwanamke wa kipekee sana, kama maandiko yanavotaja habari zake,alikuwa ni Binti mdogo sana kipindi anaolewa ,lakini kwa kipindi kifupi sana cha ndoa yake muwewe alifariki akiwa na umri mdogo pamoja na kipindi kidogo cha ndoa yake,
Luka 2:36-37
[36]Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
[37]Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
Ni jambo la kushangaza sana kwa mwanamke huyu, ijapokuwa alikuwa mjane na umri mdogo,lakini hakuona sababu ya kutafuta Kijana au mwanaume mwingine,aliona mwisho wake nitapata nini,itanifaidia nini,ni heri nimuekee Mungu tumaini langu kwa kumtumainia yeye na kumyumikia maisha yangu yote…
Na hapo tunaona akajitoa kwa Mungu Kwa kudumu katika hekalu akiomba na kusali na kufanya ibada,akitabiri na kutoa unabii mpaka Bwana anampa ufunuo wa kuja kwa Mkombozi wa ulimwengu mzima,Mungu akamtumia kuujuza ulimwengu mzima, halikuwa jambo dogo ndugu….
Luka 2:38
[38]Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
MARIAMU MAGDALENA”
Mariamu Magdalena ni mwanamke aliyekuwa na udhaifu mkubwa sana,Biblia inasema alikuwa na mapepo saba,nafikiri wote tunafahamu mapepo hata kwa kusikia,na wengi tunashuhudia kazi zao katika hu ulimwengu na katika maisha ya mtu,angalia pepo moja tu likiwa ndani ya mtu jinsi linavomfanya,linaweza kumtupa hata kwenye moto likamwangamiza,angalia pepo moja linavoweza kukufanya kuwa mzinzi na mshirikina,angalia pepo moja liavoweza kukufanya kuwa kichaa…Jiulize una mapepo saba hali yako ikoje?
Hii inatupa picha tuone Mwanamke huyu hali yake ilivyokuwa mbaya zaidi,tuseme alishazunguka hata kwa waganga akitafuta tiba lakini hakuambulia chochote ,lakini tunaona mwishowe akaona ni heri kumtumaini Mungu, heri nimtegemee Bwana…
Luka 8:2
[2]na wanawake kadha wa kadha ambao walikuwa na pepo wabaya na magonjwa wakaponywa; nao ni Mariamu aitwaye Magdalene aliyetokwa na pepo saba,
Lakini tunaona Magdalene hakuishia hapo,aliendelea kumtumaini Mungu na kuifanya kazi ya Bwana kwa uaminifu na kujitoa kwa hali na mali kuifanya kazi ya Bwana isonge mbele mpka mwisho wa Kusulubiwa kwa Bwana Yesu,,,lakini tunaona Yeye pekee ndiye wa kwanza kupewa ufunuo wa kufufuka kwa Bwana Yesu… awe wa kwanza kuutaarifu ulimwengu mzima,hii ni ajabu sana, alikuwa na moyo wa kipekee sana,sana
Marko 16:9-11
[9]Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba.
[10]Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia.
[11]Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.
Haleluya kwa Bwana Yesu Kristo……
Hayo hayakuandikwa kutufurahisha,la! Maandiko yanasema….
1 Petro 3:5
[5]Maana hivyo ndivyo wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu,
Mpaka biblia inasema “hivyo ndivyo”ni kumaanisha lazima tujifunze kwa hao wanawake ili na sisi tuige mfano wao,tujifunze kwao,tupate mashauri kwao, biblia imeshatupa njia ya watu wa kujifunza ili tuweze kumtumikia Mungu…..
Jiulize Mwanamke,dada na msichana unajifunza kwa nani,wapi unatafuta mashauri ya kumtumikia Mungu, Je ni shoga yako unategemea akushauri mambo ya rohoni,kumbuka kama hawamjui Mungu hawawezi kukushauri chochote kizuri,watakushauri uwe mzinzi, watakushauri uvae mavazi yasiyompendeza Mungu, watakuambia lazima ujipodoe upendeze,watakushauri ukimtumikia Mungu wewe ni mshamba,
“ni watu wa ulimwengu wasio mjua Mungu unaowategeme wakuongoze katika njia sahihi, ni nani unajifunza kwake….
Kama utatoka nje ya Biblia takatifu nakuhakikishia lazima ungamie tu,biblia ilishatupa watu sahihi na matokeo yake tumeona yalivyokuwa makubwa mpaka tunawasoma mpka leo,…
Ni matumaini yangu utaanza kujifunza kwa wanawake katika Biblia, mienendo yao,tabia zao,walifanyaje,lipi Zuri nilichukue na lipi baya niliondoe kwangu,
naamini ukiyatenda hayo utamwona Mungu akitembea na wewe kwa kipekee sana kama alivyotembea na Wanawake hawa tunaowasoma…………,,
Shalom,
Shea kwa wengine habari hizi njema..