Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele, Yeye aliye Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho, Aliyekuwepo, aliyeko na atakayekuja….
Nikukaribishe Dada, Binti, Mama, tuyatafakari Maneno ya Mungu wetu ili tuongeze Maarifa zaidi kila wakati….
Imetupasa tuwe watu wa kuongeza maarifa kila siku, na tunayaongeza Maarifa kwa kusoma Neno la Mungu, Biblia takatifu, Leo tutaliangalia kwa kina andiko moja ambalo limekuwa likifundishwa tofauti kabisa na Mitume walivyolivyolitoa kwa ufunuo wa Mungu,
Tulisome…
1 Timotheo 2:15
[15]Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Ulishawahi kulisoma kwa umakini mzuri hili andiko,Ukisoma kuanzia juu kwa lengo la kujifunza utagundua ni maagizo ambayo mtume Paulo aliyokuwa anayatoa kwa Kanisa la Kristo lote duniani, maagizo ambayo mwanamke apaswi kuyatenda akiwa katika kanisa,na agizo mojawapo ni pamoja na kufundisha na kumtawala mwanaume,
Lakini ukiendelea mbele kidogo unaona anatoa sababu za kwanin haruhusiwi kufanya hivyo, anazihorodhesha kwenye mstari wa 14, lakini sababu mojawapo inasema..”Mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika Hali ya kukosa” lakini hakuishia hapo anaendelea kusema,”Walakini ataokolewa kwa uzazi wake,
Ni kweli mwanamke ndiye kiumbe wa kwanza kuleta uovu na uharibifu ambao tunauona uliipindua hata dunia kwa dhambi, na kusababisha hata yale mahusiano kati ya Mwanadamu na Mungu yapotee kabisa, Maandiko yanasema mwanamke ni kiumbe dhaifu na kisicho na nguvu.
1 Petro 3:7
[7]Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.
Lakini huo haukuwa ndo mwisho wa Mwanamke, au ndo useme hauwezi kusimama kabisa katika imani kwasababu wewe ni dhaifu na usiye na nguvu, mstari wa kumi na tano anasema walakini ataokolewa kwa uzazi wake,
Hili ni andiko ambalo manabii wa uwogo wamekuwa wakilibeba na kulifundisha isivyopaswa na kuwatumainisha watu vitu ambavyo havipo katika maandiko….
Kwamba Mwanamke ni mzao mteule, na uzao wake umebarikiwa, na ataokolewa kwa uzazi wake, atadumu akibarikiwa milango ya Baraka ikifunguka katika uzazi wake, atabarikiwa na kupokea vinono katka uzazi wake….
Nataka nikuambie hayo yanaweza yakawa sawa lakini yakaja kukuletea uharibifu mkubwa kwenye maisha yako na uzazi wako pia..
Maandiko yanaema utaokolewa kwa uzazi wako, Kama, Embu tusome tena
1 Timotheo 2
[15 kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.
Jiulize Mwanamke unadumu kuwafundisha uzazi wako, (Watoto wako) kitu gani?unawafundisha jinsi ya kujipodoa na kuvaa visuruali vya kubana,unawafundisha kuimba miziki ya kidunia na matusi, mtoto wako unamfundisha nini,kumjua Mungu au kujua mambo yanayoendelea ulimwenguni
Mama unavaa mavazi ya hovyo hata mtoto wako wa kiume kukuangalia anaona aibu,unamfundisha nini,unampeleka mtoto wako disco, unawafundisha Watoto wako chuki, unapandikiza visas ndani yao…lakini mwisho wake utajikuta motoni pamoja na uzazi wako….itakuwa ni aibu sana….
Kwanini usiwe kielelezo cha wewe kuokolewa na uzazi wako,utajisikiaje umefika mbinguni na uzazi wako wote,
hata kama ni mlezi hilo ni jukumu pia la kulea, ulidumu katika upendo, kuwafundisha Watoto wako pendo la KiMungu na jinsi ya kupendana, unawafudisha imani ya kweli iliyo katika Yesu Kristo, mnadumu na uzao wako katika utakaso na kumjua Mungu,
Ukiwaelekeza njia sahihi, ukiwafundisha umuhimu wa ibadani, umuhimu wa kusoma Biblia,jinsi inavyowalazimu kuwa waombaji binafsi, nakuhakikishia hata ukiwa Haupo duniani, Maandiko yanasema hata iacha hiyo njia kamwe hata atapokuwa mzee,
Mithali 22:6
[6]Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Lakini ukimpeleka katika njia nyingine fahamu kuwa umejiangamiza wewe na uzazi wako mwenyewe,
Bwana atusaidie tuweze kuwalea watoto wetu katika misingi inayompendeza Bwana….
Shalom….
Shea kwa wengine ujumbe ………..