Karibu tujifunze Maneno ya Uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa Mabwana..
Kuna kipindi nilifikia nikaona kila kitu Nina maamuzi yangu binafsi, hata nani aniambie, anishauri bado niliona Nina uwezo wa kufanya maamuzi yangu jinsi nipendavyo, kitu ambacho kiuhalisia ni kweli, na huenda nilikuwa sawa kabisa…
Kumbe nilikuwa nakosea sana na hitimisho lake nilikuwa najiharibu mwenyewe, yaani najila nyama yangu mwenyewe, najikata nachemsha nakula, lakini mwisho wake kumbe najiangamiza mwenyewe,
Pale ambapo unaona hutaki kuambiwa chochote, unaona unafahamu kila kitu, wewe ni hodari sana, ushauri wa mtu mwingine unaona haukusaidii chochote hata kama unaona ni Mzuri na unauona ukiutendea kazi utakusaidia sana unautupilia mbali kisa wewe hakuna anaeweza kukuambia chochote kisa wewe ni msomi, mjanja sana mjuaji wa vingi inakupasa ujichunguze sana tena sana,
Kuna wakati unajiona umeshakuwa mtu mzima, unayo maamuzi yako binafsi, hakuna wa kukupangia chochote, umeshaielewa dunia, umeshajua kupambanua Jema na baya,una ujuzi mwingi hata wa kutafuta pesa katika mbinu tofauti tofauti lakini naomba ufahamu hili Unajimaliza mwenyewe,
Ndivyo ilivyo hata Katika kanisa la Kristo, Mungu aliuweka utaratibu wake wakufatwa na watakatifu wote, Kwamba Mwanamke anapokuwa katika Kanisa ni lazima afunike kichwa chake,
Embu tusome,
1 Wakorintho 11:5-6
[5]Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
[6]Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Ukisoma huo mstari wa tano anasema yuaaibisha kichwa chake, embu tafakari tena, yuaaibisha kichwa chake, kumbe unapojiona una maamuzi ya Kuja ibadani utakavyo bila kufunika kichwa na huku nywele zako ni fupi, umenyoa mitindo kama mwanaume maandiko yanasema unajiaibisha mwenyewe, unajidhalilisha mwenyewe, unajiondolea heshima yako na uthamani wako mwenyewe…
Binti, dada, Mama, unaenda Kanisani kama unaenda disco, mavazi yako hata mtu kukutazama mara mbili hathubutu jinsi yalivyo ya hovyo, unavaa suruali unasema unaenda Kanisani, unavaa sketi fupi na inampasuo, mabega yote yako wazi uvaa vikaushi, huoni aibu, unajiaibisha mwenyewe, unajidhalilisha Peke yako mwisho wake unajiangamiza mwenyewe kwenye ziwa la moto….
Ni kweli Mchungaji wako akufundishi, ni kweli unapoabudu wanakuambia njoo unavotaka Mungu haangalii mwili, ni kweli nabii wako anakuambia mwanamke ni pambo lazima ajipambe apendeze Lakini Neno la Mungu linakuambia unajiaibisha mwenyewe na kujiangamiza,
Bwana Yesu anasema,.
Hosea 4:6
[6]Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
Unaangamia kwasababu hutaki kushaurika, unajiona unafahamu sana, unasema sisi kanisani kwetu hatufundishwagi hayo, kiongozi wetu alisema hayo waliandikiwa watu wa zamani ila sio sisi, Mungu anakuona unaangamia, unajiaibisha mwenyewe….
Kubali kushauriwa leo, kubali kufundishwa,kubali kuongezewa maarifa mengine, kubali kuwa mtii,
Neno la Mungu ndio Hekima yote, ndio Maamuzi yote, ndio maarifa yote, ndio ujuaji wote, ndio mwanzo na mwisho wote,
Naamini kuanzia sasa utabadilika na kuanza kuvaa vizuri kama binti wa Mungu na kusoma Neno la Mungu na kuwa mtii wa yale Yote Bwana Yesu anayosema katika Biblia takatifu,
Shalom….
Wasambazie na wengine ujumbe hu kwa kushea…..
Amina mpendwa
🙏