SWALI: Je! Ni wanawake gani hao ambao wanazungumziwa katika katika cha Zaburi? (Zaburi 68:11)
[Zaburi 68:11]
[11] Bwana analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;
JIBU: Nakusalimu kupitia Jina la Yesu lipitalo majina yote, nakukaribisha tupate kujifunza maneno yatupayo uzima wa milele.
Wanawake wanaozungumziwa hapo ni wale wanawake ambao waliompokea Yesu Kristo katika maisha yao na kukamilisha utimilifu wote katika maandiko matakatifu, hao ndio wanawake wanaozungumziwa hapo, na wanawake kama hao Mungu anatoa ujumbe kwao kuwa watakapo peleka habari njema watakuwa jeshi kubwa, na ikiwa wakitenda kinyume na hapo watakuwa wanawake wa kawaida tu na si kama Bwana alivyolitoa neno lake
Sasa yafuatayo ni mambo kila mwanamke aliye mpokea Kristo, hana budi kuyatimiza ili awe jeshi kubwa
1.KWA KUPITIA MATENDO YAKE (YAKO)
Katika maandiko tunajifunza kwa mwanamke mmoja aliye hubiri au kutangaza habari njema kwa kupitia matendo yake, na mwanamke huyu si mwengine zaidi ya Tabitha au Dorkasi
Tusome
[Matendo ya Mitume 9:36]
[36]Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa MATENDO MEMA na sadaka alizozitoa.
Tunaona mwanamke huyu Tabitha alikuwa ni mwanamke aliye jaa matendo mema ,kwa kujitoa kwa ajili ya watu wengine na katika kupeleka injili kupitia sadaka zake, matendo yake baadae yalikuja kuwa faida kwake baada ya kupatwa na umauti, tunajifunza kuwa kupitia yale aliyo kuwa anayatenda kulirejesha uhai wake .
Jambo hili linafundisha pia kwa wanawake waliokoka, ni lazima nao wahubiri habari njema kupitia matendo yao, na si kukaa vijiweni na kuanza usengenyaji, ubea, fitina nk.. bali kutambua ni nini kusudi lake lililopelekea hadi Bwana Yesu akuite jeshi kubwa, maana huwezi kusema mimi jeshi kubwa na wakati matendo yako tu ni matatizo, watu hawakutambui kuwa umeokoka au mpagani
Matendo mengine ambayo waweza kuhubiria wengine ni katika muonekano wako wa nje, kipindi hiki tulichopo unakuta mwanamke anakwambia ameokoka na anampenda Yesu; tena kwa kukazia utambulisho wake anasema na miaka aliyonayo katika wokovu, anasema ana miaka thelathini katika wokovu, lakini ukitazama muonekano wake ni kama mtu asiyejua nini maana ya wokovu, unakuta
vimini yeye, suruali yeye, magauni mafupi, nguo zinazoonyesha maungo ya mwili wake, tena unakuta nguo hizo anazivaa kanisani, wanawake kama hawa wasijidanganye kwa kujiita jeshi kubwa, maana ni sawa na kujilisha upepo, kwa sababu Mungu wetu anatembea na neno lake tu kama ukiwa kinyume na maagizo yake hata ujipe jina kubwa katika utumishi kama utakuwa unatenda matendo yako kinyume na neno la Mungu yote ni ubatili.
Mungu atusaidie katika hili.
Maandiko yanasema katika
[1 Timotheo 2:9-10]
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
[10] BALI KWA MATENDO MEMA, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Neno la Mungu lipo wazi kabisa, hivyo basi, kwa kuwa Mungu amelitoa neno lake kwetu, basi yatupasa tusimame katika nafasi zetu kuhakikisha matendo yetu na mionekano yetu inahubiri habari njema.
2. KWA KUSHUHUDIA WENGINE HABARI NJEMA
Jambo hili ni muhimu kwa kila mwanamke aliyeokoka, maana ni AGIZO KUBWA LINALOTOKA KATIKA KINYWA CHA MUNGU, kwa maana alituachia maagizo kwa watu ambao bado hawajapata neema ya wokovu hili nao wapate kupitia sisi tulikombolewa
Maandiko yanasema katika
[Marko 16:15]
[15]Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
Ni jukumu la kila mwanamke aliyeokoka kuhakikisha anapeleka habari njema kwa kuwashuhudia wengine, na siyo mda wa kukutana katika vijiweni na kuanza kusema watu vibaya, mambo haya hayapaswi kufanyika kwa mwanamke mcha Mungu, bali anapaswa kuwahubiria wengine habari njema hili nao wabadilike watoke katika shimo la giza, hata utakapokuwa katika maeneo yoyote yawe ya kazini kwako, biashara, nk..huko huko yakupasa kutimiza wajibu wako kama jeshi kubwa, usije ukakaa na kuanza kuteta wengine vibaya, maandiko yanasema katika
[1 Wakorintho 15:33]
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
Sasa kwanini tabia yako iharibiwe na jambo kama hilo la kuteta wengine kwa kusengenya watu? Na wakati lipo jambo ambalo ukilitimiza unakuwa bora mbele za Mungu? Kwanini kujiharibia sifa njema?
Acha usengenyaji kwa kuzungumzia wengine vibaya na badala yake hubiri habari njema kwao nao wampoke YESU KRISTO.
3. KWA KUOMBA
[Yeremia 9:17]
[17]BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;
Si tu katika kutenda matendo mema na kushuhudia wengine habari njema, bali pia katika kuomba, hapo tunaona agizo linatolewa kwa wanawake waombolezaji kufika kwa ajili ya kuomboleza kwa kulia
Neno linasema
[Marko 9:29]
[29] Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba.
Yapo mambo mengine hayatoki pasipo kuomba, wewe kama wanamke lia kwa ajili ya huduma, lia kwa ajili ya kanisa, lia kwa ajili ya watumishi wachungaji, waalimu, mitume, manabii na wainjilisti ili kwamba Mungu awasimamishe wasonge mbele wasirudi nyuma, lia kwa ajili ya taifa, lia kwa ajili ya uzao wako n.k,
kupitia maombi yako itafanya kuangusha ngome zote za shetani mwaribifu, mwanamke akisimama katika nafasi hii hakika utamuona Mungu na vitu vyote vitasimama pasipo kutetereshwa na adui.
Unataka Neno la Bwana litimie kwako, basi omba
Wewe kama wanamke amka leo toka usingizini na ulisikie neno la Bwana juu yako, anza sasa kuliishi neno la Mungu kwa kutimiza kusudi la wewe kuwepo hapa duniani, acha maisha ya dhambi na na maisha ya maigizo katika wokovu
kwa kujionyesha mtakatifu sehemu maalum, lakini ukiwa nje ya hapo unakuwa mtu mwingine mwenendo huo haufai, uwe mtakatifu mahali pote iwe kazini, nyumbani, kanisani onyesha kweli umebadilishwa na Bwana Yesu
hubiri injili, tangaza kwa watu wote bila shaka wala hofu wewe ni jeshi kubwa
kaa katika KUTIMIZA KUSUDI LA MUNGU, DUNIA NA VITU VYAKE VYOTE VITAPITA LAKINI NENO LA MUNGU LITADUMU MILELE NA MILELE
AMINA
[2 Timotheo 3:16]
[16] Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Bwana Yesu Akubariki.
Mada zinginezo:
Mtupe chini Yezebeli kama unataka kuwa upande wa Mungu
BWABA YESU Awabariki sana
Amina sana
BWANA YESU AWABARIKI SANA
Amen 🙏 nawe zaidi
Amen akubariki nawe pia.
Amina
Amen