Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo,
Kwa Neema za Bwana tutajifunza somo linalohusu mapambo yasiyoharibika,
Somo na masomo haya yatakuwa yakilenga watu wote ila hasa jinsia ya kike, kwaiyo wewe kama ni dada, Binti, Mama, basi somo hili na mengine mengi yatakuwa yakikulenga kwa ajili ya kukuongezea maarifa zaidi,
Maandiko yanasema,
1 Petro 3:3-4
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
Ulishawahi kulitafakari hili andiko kwa utulivu, hapo anasema kwa mapambo yasiyoharibika, ina maana kuwa kama yapo yasiyoharibika basi kuna yanayoharibika, lakini Maandiko yametupa tuyajue yale yasiyoharibika ni yapi?
Ukisoma andiko lingine tena,anasema..
1 Timotheo 2:9
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
Jiulize Mwanamke haya ndiyo mapambo yako, Mapambo yako ni yapi? Ni make up unazopaka, ni wanja mrefu unaojiwekea,ni fasheni za mitindo ya kidunia, ni nini, ni visuruali vya kukubana na vigauni vya kuuacha mwili wako wazi, ni hayo mawigi yanayokudanganya utafanana na wazungu, n.k nataka nikuambie hayo yote ni mapambo yanayoharibika,
Makeup na poda zikipigwa na upepo zinaharibika na kuyeyuka, fasheni na mitindo inabadilika kila wakati, na kibaya zaidi haziishii kuharibika tu bali zinakuharibu mpka wewe mwenyewe na mwisho wake unajikuta katika ziwa la moto, Sasa kwanini usianze kujipamba na kutafuta kijipamba na haya mapambo ya kimbinguni.
Neno la Mungu lilishatuchagulia mapambo yetu ya kujipamba, kwamba tukijipamba na hayo tutakuwa ni watu wa thamani sana mbele za Mungu, kwanini usijipambe kwa pambo la upole ndani yako, Adabu yako iko wapi kama pambo, utulivu na watu wote umeuacha, moyo wako wa upendo uliojipamba nao uko wapi, haya na mengine mengi ndiyo mapambo yatupaso kujipamba usidanganywe na mapambo mengine hayatakupendezesha kabisa…
Hivyo pamoja kila mmoja ajitathmini mapambo yake ni yapi, kama yapo kinyume na Biblia jua hayo si mapambo bali ni machukizo,
Maandiko yanasema,.
Ufunuo wa Yohana 21:8
[8]Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Unapojipamba tofauti basi jua unamchukiza Mungu na kufanya chukizo….
Umeshapata kujua mapambo yanayokupasa kujipamba ni yapi, ni wewe kuchukua hatua ya haraka sana, na hatua ya kwanza kumbuka kama uko nje ya Kristo hutaweza kujipamba kwa mapambo hayo, hivyo yakupasa kwa moyo wako wote umwamini Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kisha utubu dhambi zako zote kwa kudhamiria kuacha pamoja na mapambo yote yanayoharibika, kisha ubatizwe ubatizo sahihi(Matendo 2:38-39)
Baada ya hapo Roho Mtakatifu ataanza kutembea na wewe na kukuwezesha kujipamba kwa mapambo ya upole na adabu na upendo ambayo ndiyo yanayompendeza…
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea