Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lisifwe…Nawasalimu nyote, natumai tu wazima kwa Neema za Bwana Yesu…
Tukaribie pamoja tuyatafakari Maneno ya Mungu wetu kila siku…..
Leo kwa Neema za Bwana tutatafakari andiko moja ambalo limekuwa likijulikana na wengi na kufahamika sana,,lakini kuna namna nyingine ambayo Bwana anatamani tuifahamu maana Biblia inasema…
Zaburi 12:6
[6]Maneno ya BWANA ni maneno safi,
Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi;
Iliyosafishwa mara saba.
Basi kwa kwa pamoja twende moja kwa moja kwenye somo letu linalosema, Waacheni watoto wadogo, na neno hili tunalipata katika kitabu cha..
Marko 10:13-14
[13]Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse; wanafunzi wake wakawakemea.
[14]Ila Yesu alipoona alichukizwa sana, akawaambia, WAACHENI WATOTO WADOGO WAJE KWANGU , MSIWAZUIE; KWA MAANA WATOTO KAMA HAWA UFALME WA MUNGU NI WAO..
Haya ni maneno ya Bwana Yesu mwenyewe wakati analetewa jopo la watoto wengi ili azungumze nao chochote, lakini tunaona baadhi ya wanafunzi wakaanza kuwazuia baadhi ya hawa wazazi, au walezi..Pamoja na kuwazuia lakini tunaona kitendo hicho hakikumpendeza Bwana na mwishowe tunaona alichukizwa..
Pamoja na hayo yote mwishowe tunaona Bwana anatoa hitimisho la mzozo huo ambao tunausoma katika mstari wa 14, Kwamba..Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wao….
Mama, Mlezi, Mwanamke ulishawahi kutafakari hu mstari kwa utulivu ili ujue hatma ya maisha ya mtoto wako, ulishawahi kukaa chini na kumruhusu Roho Mtakatifu akufunulie zaidi …ukisoma hapo anasema waacheni watoto wadogo alafu ukiendelea mwisho anamaliza kwa kusema kwa Maana ufalme wa Mungu ni wao,…..Kumbe ufalme wa Mungu unaanza katika hali ya udogo sana, kumbe ufalme wa Mungu unaumbika ndani ya mtu Katika Hali ya chini kabisa….
Jiulize Mama watoto wako,…. katika hali hiyo ya udogo waliyonayo umepanda nini ndani yao, je ni nyimbo za kidunia, ni kila siku kuwapeleka kwenye matamasha ya kuangalia muvi, ni staili mpya za kunyoa na kusuka, ni katuni za ajabu ajabu unazowawekea kila wakati, ni nini unawafundisha…..Kumbuka hayo na mengine mengi ndiyo yanayomchukiza Bwana….
Maandiko yanasema….
Mithali 22:6
[6]Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Kwanini katika hali hiyo ya udogo, hali ya kutoweza kupambanua mambo, hali ya udogo ya kutokuweka vitu akilini kwake, ukaitumia wewe Mama kumfundisha na kumpandia ndani yake habari za ufalme wa Mungu, habari za Upendo,habari za msahama na huruma, habari za kuomba na kusoma Biblia….
Mtengenezee Bwana njia safi na nzuri ya kumtumia mtoto wako hata Katika Hali ya udogo aliyo nayo, kama alitumia punda kusema na Balamu,itakuwaje kwa mtoto mdogo mwenye ujuzi wa siri za Ufalme wake,hapo maandiko yanasema, Msiwazuie,na zaidi sana anaendelea kusema,,Kwa maana watoto kama hawa,,utajuliza ni watoto wapi,ni hao uliowatengeza katika misingi mizuri ya kumjua Bwana katika udogo wao.. na Bwana anaona vema kuwapa ufalme wake….
Badilika mwanamke, Anza kumfundisha na kumtengeza mtoto wako katika misingi bora ya Neno la Mungu, hataiacha hata atakapokuwa mzee
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea….
Shalom
Mada zinginezo
WALAKINI ATAOKOLEWA KWA UZAZI WAKE
PASIPO MIMI NINYI HAMWEZI NENO LOLOTE
Mtupe chini Yezebeli kama unataka kuwa upande wa Mungu
Amina
Ubarikiwe na Bwana