Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lisifiwe milele na milele…..
Karibu tujifunze Maneno ya uzima…..
Ilimpendeza Mungu kuachia Neno lake kwa njia ya maandishi ili itusaidie sisi…ni sawa na mtu aliyeandika waraka ukasomwe mahali fulani, kuonyesha ni neno lake lilelile ila kalieka kwa njia ya uandishi…..basi imetupasa tuwe watu wakulisoma sana Neno lake ili tupate kuelewa ni nini anasema na sisi…
Yapo Maneno mengi Bwana aliyoyazungumza kipindi yupo ulimwenguni…embu twende tukasome baadhi ya maneno yake…..
Tusome….
Yohana 15:5
[5]Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Yazingatie maneno yaliyokolezwa sana….
Umeona hapo ,,mpaka mtu anakwambia maneno kama hayo anaujasiri wa kutosha, anaufahamu kwelikweli, si amekurupuka tu huko, ni anauelewa na kile anachokiongea….embu tujifunze kwa mfano wa maisha kidogo…
Wote tulishapitia hali za kuwa watoto wadogo na mpaka tumekuwa watu wazima…sasa rudi nyuma kipindi ukiwa mtoto, kipindi huna mawazo yoyote kwenye akili yako, hufikirii hata kesho itakuwaje wala utakula nini, huna fikra za kwamba kuna kushindwa we kwako unaona mambo yote yanawezekana….n.k….hayo yote hayakuja ndani yako tu wala hayakujiumbia yenyewe….hayo yote yalikuja kutokana na wazazi wako kufahamu kuwa pasipo wao wewe hauwezi chochote…
Ndipo hapo wakaanza kukuwekea imani hiyo kwako wakijibidiisha ili usikose maziwa, usikose chakula, chochote utakachotaka wahakikishe unakipata kwa wakati, walifahamu hilo mapema kwamba huwezi lolote pasipo wao….
Mama, dada, binti….ni mara ngapi umeisikia injili umeipuuzia,,umehubiriwa mara ngapi kwamba hivo visuruali, na visketi vifupi na vitop unavyovaa ni machukizo kwa Mungu lakini hubadiliki….Hayo mapambo unayojiwekea huoni unaupinga uumbaji wa Mungu, ni lini utaacha umbea na usengenyaji,hayo matusi unayotukana huoni unamkoea Bwana Yesu…hao wanaume za watu utatembea nao mpka lini huoni unafanya uzinzi mbovu…
Geuka sasa ndugu yangu,,yakupasa ufahamu hili … kwa nguvu zako mwenyewe hutaweza,ndo mana uliposikia maneno haya kuna namna unatamani utoke huko lakini unajikuta huwezi,,leo unatoka kesho unarudia hali ile ile,hiyo NGUVU HAUNA..
Maandiko yanasema……
Matendo ya Mitume 1:8
[8]Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
Lazima hii nguvu ikae ndani yako ili uweze kuishinda dhambi,sasa utajiuliza nitaipataje hiyo nguvu na Roho Mtakatifu…………..
Bwana Yesu anaendelea kusema,,,,
Matendo ya Mitume 2:37-39
[37]Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
[39]Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.
Umeona eeh…..waliposikia habari kama hizi ulizozisikia wewe, walitamani watoke huko kisha wapokee nguvu…na njia ni moja tu lazima watubu dhambi zao zote wakimaanisha kiziacha kabisa….baada ya hapo lazima wabatizwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo sawa na maandiko,ili usafishwe dhambi zako zote na upokee Roho Mtakatifu ambaye ndiye Nguvu ya kukusaidia usirudi nyuma tena…
Unasubiri nini tena,kwanini uteseke katika dhambi,kwanini ufe na dhambi zako ukachomwe katika ziwa la moto upotee milele…Chukua maamuzi sahihi wakayi hu…
Mkimbilie Yesu Kristo ,yeye ndiye kweli na uzima…..Hakuna wokovu kwa mwingine awaye yoyote…
Yohana 6:37
[37]Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea…..
Shalom….