Kama upo msimu wa mvua, kuota unanyeshewa na mvua ni jambo la kawaida kwasababu biblia inasema..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi..”
Kwahiyo ni kawaida kuota lile jambo linalochukua nafasi kubwa katika fahamu zetu au maisha yetu.
Lakini kama haupo msimu wa mvua na umeota unanyeshewa na mvua. Ni ishara ya NEEMA YA MUNGU.
Zaburi 68:9 “Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu”.
Vile vile maandiko yanasema..
Hosea 6:3 “Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujilia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi”
Na tena..
Yoeli 2:23 “Furahini, basi, enyi wana wa Sayuni, mkamfurahie BWANA, Mungu wenu; kwa kuwa yeye huwapa ninyi mvua ya masika, kwa kipimo cha haki, naye huwanyeshea mvua, mvua ya masika, na mvua ya vuli, kama kwanza”.
Kwahiyo ni ishara nzuri, lakini ili baraka hizo na Neema hizo zije Idhihirike au zitokee, ni lazima ukae katika sheria zake na amri zake. Lakini kama hutadumu katika kufanya mapenzi ya Mungu ndoto zako hazitatimia haijalishi ni Mungu kakuonesha, hazitatimia!, Hiyo ni kulingana na biblia.
Maran atha!
[…] KUOTA UNANYESHEWA NA MVUA […]
[…] KUOTA UNANYESHEWA NA MVUA […]