Kama kazi yako ni ya shambani au katika bustani, kuota unachuma matunda ni jambo la kawaida..kwasababu biblia inasema..
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…”.
Lakini kama kazi yako si ya mashambani, na umejikuta umeota ndoto kama hiyo, upo unachuma matunda katika mti..
Ni ishara ya kwamba mafundisho unapokea kutoka kwa mtu/ watu ambao aidha ni watu wa Mungu au watu wa shetani.
Ukiona unachuma matunda kwenye mti ambao una matunda mazuri na hauna dosari yoyote basi ni ishara kwamba mahali ulipo Mungu anakulisha matunda mazuri ya rohoni kupitia mtu fulani ambaye ni mtumishi wake.
Lakini ukiota unachuma matunda ya mti ambao matunda yake si mazuri, aidha yameoza au ni ya mwitu, au ukiona mti huo una dosari ya miiba au ina viumbe vya hatari kama nyoka, au kenge au mijusi , hiyo ni ishara kwamba, kuna mafundisho unayapokea ambayo ni hatari kutoka kwa watumishi wa shetani au pengine wewe mwenyewe unajiaminisha vitu kutoka katika fahamu zako ambavyo ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Maandiko yanasema..
Mathayo 12:33 “Ufanyeni mti kuwa mzuri na matunda yake kuwa mazuri; au ufanyeni mti kuwa mbaya na matunda yake mabaya, kwa maana kwa matunda yake mti hutambulikana.
[34]Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.
[35]Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema; na mtu mbaya katika akiba mbaya hutoa mabaya”.
Umeona?.
Kwahiyo hiyo ni ndoto ya tahadhari, kuonesha kuwa ujihadhari na manabii wa uongo
Mathayo 7:15-20
[15]Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.
[16]Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
[17]Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
[18]Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
[19]Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
[20]Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Na vile vile jiangalie na wewe mwenyewe matunda unayotoa.
Kama hujaokoka ni vyema ukaokoka ili Bwana Yesu ayasafishe maisha yako na uanze kuzaa matunda mazuri.
Bwana akubariki
Whatsapp -0789001312