Menu
NDOTO ZANGU
  • Home
  • Orodha ya Ndoto
  • Quizzes & Surveys
  • Contant
  • English Articles
  • Kuhusu
  • MASOMO KWA WANAWAKE
NDOTO ZANGU

KUOTA UNAJENGA NYUMBA

KUOTA UNAJENGA NYUMBA.

Posted on December 13, 2021

Nini maana ya kuota unajenga Nyumba, ngome, mji au mnara?

Ndoto hizi zimegawanyika katika sehemu kuu tatu , 1) Unaota unajenga nyumba lakini haiishi, au unaishia katikati 2) Unaota unajenga nyumba inakamilika lakini baadaye inaanguka au unanyang’anywa. 3) Unaota unajenga nyumba na inakamilika vizuri.

Tutaangalia kundi moja baada ya lingine.

  1. Unaota unajenga nyumba lakini haiishi.

Kama wewe umempokea Yesu, (yaani umeokoka vizuri) na kisha ukajikuta umeota ndoto ya namna hii, basi kuna uwezekano mkubwa sana, ikawa ni ujumbe wa Mungu kwako.

Nyumba au kitu chochote mtu anachoweza kukijenga siku zote vinawakilisha “Huduma ya Mtu” au “Wito wa Mtu”. Mtu aliyeitwa na Mungu na kuanza kumtumikia katika nafasi yoyote Mungu aliyomweka, katika roho ni sawa na anajenga nyumba au mnara au ngome. Hivyo kila mtu anajua jinsi anavyoijenga nyumba yake, wako walio hodari na walio dhaifu. Mtu dhaifu ni Yule ambaye hayupo makini na wokovu wake, katika roho anakuwa anaijenga nyumba yake kilegevu. Na inapotokea kaacha kabisa wokovu au karudi nyuma, basi katika roho nyumba yake hiyo inakuwa imesimama haiendelei kupanda, ndicho Bwana Yesu alichosema katika..

Luka 14:27 “Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?

29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki,

30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza”.

Kwahiyo ni lazima kuhakikisha unapiga gharama zote kabla ya kumfuata Bwana Yesu, vile vile unajikana nafsi katika kuishi maisha ya kikristo, ulegevu wa aina yoyote baada ya kumfuata Yesu, inatafsirika kiroho kama kazi iliyosimama

2) Unaota unajenga nyumba inakamilika lakini baadaye inaanguka au unanyang’anywa.

Nyumba kuanguka ni kuonyesha kuwa haikujengwa katika msingi ulio imara, maana yake ni kwamba, Mafundisho ya awali mtu aliyoyapokea kumhusu Yesu yalikuwa dhaifu, au mtu huyo hakumwelewa Bwana Yesu kama alivyopaswa kumwelewa, au aliyachukulia juu juu tu maneno ya Bwana Yesu, na akaendelea hivyo hivyo, katika kumtumikia Mungu..

Mathayo 7:26 “Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;

27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa”.

     3) Unaota unajenga nyumba na inakamilika vizuri.

Kuota unajenga nyumba na inakamilika na inadumu, ni ishara nzuri kuwa Huduma yako inaendelea vizuri au itaendelea vizuri katika roho,  Lakini kwasababu ujumbe umekuja kwa njia ya ndoto, bado inakuwa ni tahadhari kwamba, huna budi kudumu katika imani, ili mambo hayo yatimie kama ulivyoyaona, shetani asiyaharibu, Kwasababu biblia inasema.

Ufunuo 3:11 “Naja upesi. Shika sana ulicho nacho, asije mtu akaitwaa taji yako”.

Ikiwa bado hujampokea Yesu na umeota ndoto hizo na kwa bahati umekutana na ujumbe huu, basi Bwana amekukusudia uokoke ili ushiriki Baraka zake. Mpokee Yesu na ukabatizwe.

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts

  • MTIHANI WA BIBLIA (part 1)
  • KWA NENO LAKO, nitazishusha nyavu”
  • UKO WAPI? Mwanzo 3:9
  • UTAOKOKA LINI?
  • BWANA AKALIZIDISHA KANISA KWA WALE WALIOKUWA WAKIOKOLEWA

Recent Comments

  1. Goodluck on MASWALI YA KITABU CHA ISAYA
  2. Magdalena on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  3. Goodluck on SITIRI MWILI WAKO, USIWE CHANZO CHA MWENGINE KUTAMANI
  4. Goodluck on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  5. Magdalena on USIMNAJISI BINTI YAKO, ILI KUMFANYA AWE KAHABA.

Archives

  • March 2023
  • February 2023
  • January 2023
  • December 2022
  • November 2022
  • October 2022
  • September 2022
  • August 2022
  • June 2022
  • May 2022
  • April 2022
  • March 2022
  • February 2022
  • December 2021
  • November 2021

Categories

  • Ndoto kutoka kwa Mungu.
  • Ndoto za Adui (shetani)
  • Ndoto za tahadhari.
  • Uncategorized
  • Wanawake

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2023 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress