Nakusalimu kwa jina la Mkuu wa ulimwengu hu na ule ujao YESU KRISTO….ni Neema kwetu kuiona siku mpya kwa maana lipo kusudi ndani yake….
Karibu tuyatafakari Maneno yake ya uzima ambayo ndiyo taa na mwanga wa maisha yetu…
Kuna vitu sisi wanadamu tukivifanya na kuviona havina umuhimu kwetu ni rahisi kuachana navyo au kuvikatia tamaa kabisa, au kutafuta namna nyingine ambayo itakuwa bora sana kwa wakati huo…kwa uhalisia mpaka unafikia hatua hiyo ni kuonyesha hakuna faida yoyote utakayopata hata ukiendelea katika mambo hayo….
Ndivyo ilivyo na Katika UKRISTO, swali linakuja UMEPATA FAIDA GANI?
Dada, binti, toka unavaa visuruali vya kubana mpaka leo,umefaidika na nini,ni kuyachora maumbo yako, faida yake iko wapi, ni kuambiwa umependeza na hao walevi…ni nini basi umepata toka unavaa mawigi ya bandia hata leo, umefaidika na faida sh ngapi, ni nini umepata unapojipaka marangi usoni,umepata faida gani mpaka sasa, ni ili ufanane na nyumba kwa huo mchanganyo wa rangi zako….
Umepata faida gani kwa uzinzi unaoufanya, faida gani umefikisha toka uanze kutembea na wanaume za watu, ni huo ugonjwa wa ukimwi unaokutafuta…Umepata faida gani”umefaidikaje na hizo pombe za hovyo unazokunywa, toka uanze kukesha bar na kwenye madisco ya vichochoroni umepata faida gani, ni nini umepata, ni huko kujulikana kwa jina la Chapombe….
Faida yako iko wapi, unapowasengenya wengine, unapowazungumzia mabaya na kuwaombea kifo, umepata nini…je wewe umekuwa mwema sana..ni nini imeongezeka kwako,,,umepata faida gani, unapowaendea kwa waganga uwaloge na kuwarudisha nyuma wengine, ulipata faida asilimia ngapi….fedha zako zimeisha au zimeongezeka…Umefaidika na nini……
Umepata faida gani toka uanze kutukana,imekufaidia nini unavyowatukana mpaka waliokuzidi umri, umepata faida gani…kijiji kizima kinakuchukua kwa tabia zako mbovu, umefaidika wapi hapo…umepata faida gani, unavyowadharau na kuwajibu wazazi wako vibaya hivyo…faida yako iko wapi…ni hiyo laana inayokimbizana na wewe, umepata faida gani…nionyeshe faida yako….Umepata faida gani…
Maandiko yanasema….
Marko 8:36
[36]Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?
Itakufaidia nini kupata kila kitu alafu mwisho ukachomwe katika ziwa la moto…Itakufaidia kitu gani ewe dada, ewe Mama, ewe binti………
Badilika sasa, wakati wa kugeuka ndio hu…maanisha kutubu kabisa ndani ya moyo wako kwa kumkabidhi Yesu Kristo Maisha yako ili akusafishe uwe kiumbe kipya na ufanyike kuwa mtoto wa Mungu…..
Maanisha sasa ili uzipate faida zote za kwenda Mbinguni……
Wasambazie na wengine habari hizi njema kwa kushea…Bwana akubariki…
Shalom…….