Kama ulikuwa unawaza au kufikiri sana habari ya kuwa na mtoto, basi ni kawaida kuota ndoto za kujifungua kwasababu ndio kitu kinachoendelea kwa wingi katika mawazo yako na akili zako .
Biblia inasema.
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;……”.
Hivyo ndoto ya namna hii inapokujia ipuuzie tu!, kwasababu ni wanawake wote wenye mawazo hayo, huwa wanaota hizo ndoto..
Lakini kama ulikuwa hujawahi kuwaza kuwa na mtoto hivi karibuni na hayo mawazo hayakuwepo kabisa kwenye akili yako, na ghafla tu unajikuta unaota hiyo ndoto, na hata wakati mwingine unaota zaidi ya mara tatu au nne, basi tafsiri yake ni kwamba kuna jambo zuri linakwenda kuzaliwa katika maisha yako, hususani katika ile shughuli unayojishughulisha nayo sana. Aidha katika huduma yako ya kuhubiri inayoifanya, au shughuli yako ya mikono au pengine hata kukutana na mtu sahihi ambaye atakuoa na kupata mtoto.
Tendo la kuzaa ni ishara kwamba mimba ilishatungishwa huko nyuma, hivyo kuzaa ni hitimisho tu la tendo ambalo tayari lilikuwa limeshaanza kutendeka huko nyuma.
Luka 1:30 “Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Lakini kama bado haujaokoka na umeota ndoto ya namna hii basi ni ishara kuwa kuna jambo litakwenda kuzaliwa mbele yako ambalo si zuri.
biblia inasema..
Ayubu 15:35 “Wao hutunga mimba ya madhara, na kuzaa uovu, Nalo tumbo lao hutengeza udanganyifu”.
Zaburi 8:14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo”
Yakobo 114 “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Umeona matunda wanayoyazaa watu waovu?..siku zote si mazuri..
Mathayo 3:10 “Na shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni”.
Hivyo ni wakati wa kujiangajlia na kujitathmini matunda utakayoyazaa.. Kama ni mwenye dhambi maandiko yanasema.. Mshahara wa dhambi ni Mauti, na tena yanasema..
Yakobo 1:15 “Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti”.
Lakini jambo la faraja ni kwamba Bwana Yesu leo anaokoa, na zaidi sana anaweza kutufanya tumzalie matunda mazuri yanayodumu. Mpokee leo na kubatizwa nawe utazaa matunda mazuri.