Ndoto ya kuota unaokota hela inaweza gawanyika katika makundi mawili ambayo ni,
1) Kuota unaokota Sarafu
2) Kuota unaokota noti.
Ndoto yoyote inayohusisha kuokota fedha, haina maana nzuri kama inavyotegemewa.
Fedha ya kuokota haina tofauti na fedha ya wizi, uchungu anaoupata mtu aliyepoteza fedha hauna tofauti na yule aliyeibiwa, hivyo kuokota pesa sio jambo la ushindi sana.
Sasa inapotokea umeota unaokota fedha za noti, maana yake ni kwamba kuna fedha ambazo unazitamani au zitakujia ambazo sio njema, na ni nyingi kidogo ambazo zitasababisha uchungu kwa upande mwingine, na mara nyingi fedha hizo zinakuwa ni za rushwa, au kupewa na mtu aliyeiba, au kupewa na mtu ambaye kazipata kwa njia isiyo halali, iliyosababisha uchungu kwa mwingine.
2) Kuota Sarafu
Unapoota unaokota sarafu, tena wakati mwingine zimejioanga mstari mmoja, tafsiri yake ni hiyo hiyo kama ya fedha za noti, isipokuwa, sarafu inawakilisha uchache wa fedha, maana yake kuna fedha ambazo si nyingi sana zitakujia au zimeshaanza kukujia ambazo si safi.
Fedha za namna hiyo hazina baraka yoyote kutoka kwa Mungu zaidi ya laana.
Hivyo uonapo mazingira kama hayo yanatokea katika maisha yako, mazingira ya kupewa au kupata fedha isiyo halali, iwe nyingi au kidogo, ambayo itasababisha uchungu kwa mwingine mfano ule ule wa mtu aliyeibiwa fedha au kutapeliwa..huna budi kuikwepa na kuwa mtu wa haki, kwasababu biblia inasema..
1 Timotheo 6:10 “Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi”
Na zaidi sana inasema achumaye kidogo kidogo atafanikiwa.
Mithali 13:11 “Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa”.
Kwahiyo hiyo ni ndoto ya tahadhari.
Je unazijua faida za kuokoka?..Zijue faida kadhaa za kuokoka kwa kobofya hapa > Nini kinatokea siku unapookoka?