1.Je amri ya pili ni inasemaje?
______________
2. Je ni watu gani ambao Paulo aliwaandikia kuwa wamelogwa?
______________
3.je ni mtoto gani wa Daudi aliye uliwa na Sulemani?
_________________
4.Elisha alikufa kifo gani?
__________________
5.je ni nabii gani aliye simamisha mvua kwa miaka mitatu na nusu?
___________________
6.wana wa kuhani Eli wanaitwa wakina nani?
__________________
7.je Amri ya 7 inasemaje?
_________________
8.je mfalme sauli alipo weka nadhili kuwa asile mtu wawapo vitani je ni nani aliye kula akalifedhehesha jeshi?
___________________
9.je Shimei alimkosea nini Mfalme Daudi?
___________________
10. Kwanini Absalomu alikamatwa mapema.
___________________
Nakutakia mtihani mwema .
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618
04/03/2023
MASAHIHISHO YA MTIHANI LEO
MTIHANI WA BIBLIA (part 16)
(MASWALI YA BIBLIA)
1.Je amri ya pili ni inasemaje?
Jibu. Kutoka 20:4-6
[4]Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
[5]Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
[6]nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
______________
2. Je ni watu gani ambao Paulo aliwaandikia kuwa wamelogwa?
Jibu. WAGALATIA
Soma. Wagalatia 3:1
______________
3.je ni mtoto gani wa Daudi aliye uliwa na Sulemani?
Jibu. ADONIA
Soma. 1wafalme 2;19-25
_________________
4.Elisha alikufa kifo gani?
Jibu. Alikufa kwa ugonjwa.
Soma. 2Wafalme 13;14-20
__________________
5.je ni nabii gani aliye simamisha mvua kwa miaka mitatu na nusu?
Jibu. NABII ELIYA MTISHBI
Soma 1Wafalme 17;1
___________________
6.wana wa kuhani Eli wanaitwa wakina nani?
Jibu. Finehasi na HOFNI
Soma. 1Samweli 1;3
__________________
7.je Amri ya 7 inasemaje?
Jibu. Usizini
Soma. Kutoka 20;14
_________________
8.je mfalme sauli alipo weka nadhili kuwa asile mtu wawapo vitani je ni nani aliye kula akalifedhehesha jeshi?
Jibu. YONATHANI
Soma.1Wafalme 14;26-27
___________________
9.je Shimei alimkosea nini Mfalme Daudi?
Jibu. ALIMLAANI DAUDI PASIPO KOSA.
Soma. 2Samweli 16:5-14
___________________
10. Kwanini Absalomu alikamatwa mapema.
Jibu. Nywele zake zillikuwa ndefu sana hivyo zilinasa kwenye mti.
Soma. 2Samweli 18;9-15
___________________
BWANA YESU akubariki sana shea na kwa wengine pia.
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618