Utukufu na heshima na zirudi kwake Bwana wetu Yesu Kristo, yeye aliyetupa Neema ya siku nyingine na uhai tele…Sifa ni zake milele…
Nakukaribisha tuendelee kujifunza maneno ya Uzima wetu…
UTAOKOKA LINI?
Hili ni swali ambalo mwanadamu yoyote aliye na pumzi ya Mungu anatakiwa kujiuliza kila wakati, swali hili haliangalii dini yako, na wala halijalishi kama una imani gani, au ni kilema, au ni maskini, una uwezo, au una upungufu wowote wa akili n.k, kila aliyeumbwa kwa sura ya Mungu yakupasa ujiulize sana….
Swali ni kwanini?
Kwsababu Wokovu ndio hatma ya mwisho ya Maisha yako hapa duniani, na hata ukiondoka katika huu ulimwengu..Matendo ya swali hilo ndiyo yatakayokupa wewe tiketi ya kujua ulikuwa upande gani…
Lakini inashangaza wanadamu wa leo, ukiwauliza swali hilo hilo,,utaokoka lini?…bila shaka kila mmoja atakuwa na jibu lake, mwingine atakuambia ngoja nimalize ujana kwanza, mwingine atakujibu nikikaribia kuzeeka ndio nitaokoka,Wengine watakuambia haina haja Kwa sababu tulishakombolewa Msalabani, tunaishi kwa Neema, kuna mmoja aliniambia Yesu akikaribia kurudi na mimi ndo nitaokoka, yaani kwa ufupi kila mmoja anakuwa na sababu zake. Lakini Maandiko yanasemaje::
2 Wakorintho 6:2
Wakati uliokubalika nalikusikia,
Siku ya wokovu nalikusaidia;
tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.)
Pale unapoona unazo sababu elfu za msingi za wewe kutokuoka, maana yake ni kuwa, Biblia inaziona sababu zako si kitu chochote, Bwana Yesu mwenyewe anakuambia saa ya kuokoka ndiyo sasa na si badae wala kesho, saa ya kutoka katika maangamizi yatakayoikuta hii dunia ni sasa, usisubiri yatokee ndo utafute njia ya kusaidia, kwani utakuwa umepotea kabisa…
Maandiko yanaendelea kusema..
Mithali 6:10-11
[10]Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
Bado kukunja mikono upate usingizi!
[11]Hivyo umaskini wako huja kama mnyang’anyi,
Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.
Kwanini usichukue maamuzi sasa hivi ndugu yangu, utaendelea kuwa mtenda dhambi hata lini, utakuwa mzinzi na kuuharibu mwili wako mpaka wapi, embu jiulize leo UTAOKOKA LINI, Bwana anasema saa ya kuokoka ni sasa hivi, kwa sababu hujui yakayo kukuta hata dakika sifuri mbele, Umeanguka gafla na ukafa, embu fikiria huko unakokwenda utakuwa mwenyeji wa nani, Mungu Muumba wako humjui, humjui yo yote yule, nani atakupokea wewe? Sasa Kwanini hayo yakukute wakati nafasi ya kutosha kuanza upya na Mungu unayo sasa? Mambo ya dunia yanapita ndugu zetu, hakuna aliyekuja na kitu na kurudi nacho..kwanini usithamini maisha yako….
Mkaribishe Yesu Kristo katika maisha yako awe Bwana na mwokozi wa roho yako, bado ujachelewa, kataa kuwa mkia kwenye swala la muhimu kama hili, mkimbilie Kristo msalabani leo, Yeye ndiye njia na uzima, hakuna wokovu kwa awaye yote isipokuwa Yesu Kristo, hakuna kabisa…
Tubu leo dhambi zako kwa kumaanisha kabisa kuziacha, na kisha ukabatizwe ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo…Utapokea Roho Mtakatifu atakayekuongoza katika njia zako zote…Ni rahisi sana na hakuna gharama yoyote ukitaka kuokoka….
Saa ya wokovu ndiyo sasa…
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea……