Shalom,Bwana Yesu Kristo asifiwe..Karibu tena tujifunze Maneno ya Mungu…
Mwanzo 3:9
[9]BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
Kabla ya Uovu kuingia pale eden ukaribu wa Mungu na Adamu ulikuwa ni mkubwa sana.. kama tunavyofahamu habari yenyewe,kulikuwa hakuna haja ya kuitana itana kila wakati,Maandiko yanatuonyesha Mungu alipokuwa akitaka kuzungumza na Adamu alikuwa akashuka na kuongea naye na kupanga mipango yao…
Ni kama wakati huu, baba yako anajua kabisa wewe ni mwanae na anajua ni wapi mahali anaweza kukukuta, hivyo hana haja ya kuhangaika sana au kusumbuka sana ni wapi nitaongea na mwanangu wakati anajua makazi yako halisi ni nyumbani kwake…na hata pia akijua kuna jambo ulilifanya baya atakusubiri huko huko ili akuonye ijapokuwa wewe utakuwa na hofu nyingi kwa kosa ulilolitenda..
Ndivyo ilivyokuwa kwa Mungu na kwa Adam…kulikuwa na uhusiano mkubwa kati ya Baba na mtoto.. ndo mana kwa Adam hakuwa na hofu wala Mashaka wala wasiwasi wowote kuongea na Mungu…
Lakini Gafla tunaona baada ya uovu/dhambi kuingia katikati yao, ule uhusiano wa Baba na Mtoto ukapotea mara moja,Mungu anaanza kumtafuta tena Adam,anaita Adam uko wapi,…Mungu anashangaa anashuka aongee na mwanae wapange mipango yao anashangaa amwoni tena…..wewe unafikiri mpaka kitendo cha Mungu kumwita Adam kilikuwa ni masihara ,hapana, alikuwa kweli amwoni mwanae kwenye ule uwepo wa toka mwanzo aliouzoea…ndo mana ikambidi atafute njia mbadala ya kumpata Adam….ndo hapo anamwita na kumuulizia..
Lakini tunakuja kuona Majibu ya Adamu baada ya kusikia sauti ya Mungu..
Mwanzo 3:10
[10]Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Na Wanadamu wote tumetoka viunoni mwa wazazi wetu wa kwanza,ndo mana mpaka sasa tunazaliwa na dhambi ijulikayo. Kama ya asili,…..
Tunajifunza nini
Hata sasa Mungu anaita watoto wake,bado anaita “Uko wapi”, nia ya Mungu kukuita si wewe uanze kujielezea kama Adamu na kutoa sababu za msingi…lengo la Mungu ni ili ayarudishe yale mahusiano tena yaliyopotea kati ya Baba na mtoto…Mungu anaona mbona mwanangu nipo mbali naye,mbona simuoni mtoto wangu katika njia zangu zozote,mwanangu ameniacha,amenisahau mimi baba yake,hanikumbuki….ndipo hapo huruma za Mungu zinashuka na kuanza kukuita….
Leo hi watu wamemwacha Mungu wa kweli Muumba mbingu na nchi wanaabudu sanamu,miti,vitu walivyovichonga kwa mikono yao,watoto wamemuacha Baba yao aliyewapa pumzi na uzima wameenda kujishukamanisha na baba wa ulimwengu huu shetani, Wanadamu wamemkataa Mungu mwenyezi na kuvikubli vitu vya dunia hii na kuvitumikia…wengi wa leo ukiwaambia habari za neno la Mungu ni kama unawapa habari mpya na wengine hawataki kabisa kuzisikia…wamefarakana na Mungu,hawataki uhusiano naye kabisa…wengine wamejiundia miungu yao na kuiabudu…lakini sauti ya Mungu bado inaita…inakutaka wewe uliye mbali naye usogee karibu mzungumze kama baba na mwanae,sauti ya Mungu bado inakuita utoke huko kwenye vifungo vya dhambi ili akufanye kuwa huru.. sauti ya Mungu inaita ikksema uko wapi mwanangu,sauti ya Mungu inakutana urudi uweponi mwake…
Adamu alisikia sauti ya Mungu akaijificha kwasababu ya dhambi zake…lakini sisi tumepata Neema kwa Yesu Kristo Mwokozi….maandiko yanasema
Isaya 1:18
[18]Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
Usiwe mtoto mkaidi,isikie sauti ya Mungu inayosema nawe, Sauti ya Mungu inakutaka wewe utubu dhambi zako,sauti ya Mungu inakutaka ukabatizwe na kupokea Roho Mtakatifu ili yale mahusiano yaweze kurudi upya tena…isikilize hi sauti….
Yohana 10:27-28
[27]Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
[28]Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Usifanye moyo wako mgumu,wale wanaompenda Mungu wataisika sauti yake inayoita kila wakati…na Bwana anasema kondok wake lazima waisike sauti yake…ikkwa wewe ni mtoto wa Mungu isikie sauti ya Baba inayokuita leo…
Mkimbilie Yesu Kristo leo….
Shalom…
Wasambazie wengine habari hizi njema kwa kushea….