Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe, nakukaribisha tena tujifunze Neno la Mungu linalotupa uzima wa milele na uhakika wa maisha yetu baada ya kufa kama Neno Mwenye alivyosema kwenye
Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. YEYE ANIAMINIYE MIMI, AJAPOKUFA, ATAKUWA ANAISHI;
Biblia inasema katika
Luka 6:39 Akawaambia mithali, Je! Aliye kipofu aweza kuongoza kipofu? Hawatatumbukia shimoni wote wawili?
Katika siku hizi za mwisho, watu wengi katika kanisa wapo chini ya viongozi vipofu ambao mwisho wao wote ni shimoni, Sasa unaweza uliza ni vipofu wa nini? Jibu ni kwamba, hawa ni vipofu wa neno la Mungu (injili ya Kristo), ambayo haijawazukia ndani yao kwa kukataa kuitii wakidhani biblia haipo sawa au inajichanganya hivyo kupelekea kutumia elimu zao na hisia zao kuelewa neno la Mungu, ndugu mpendwa, hicho kitu si kweli, neno la Mungu ni safi, ni kama fedha iliyosafishwa kalibuni mara sana juu ya nchi
Zaburi 12: 6 Maneno ya BWANA NI MANENO SAFI, Ni FEDHA ILIYOJARIBIWA KALIBUNI JUU YA NCHI; ILIYOSAFISHWA MARA SABA.
Na tena neno la Mungu limehakikishwa
Mithali 30:5 KILA NENO LA MUNGU LIMEHAKIKISWA; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
Hivyo basi, Kwa kuwa neno la Mungu halijichanganyi ni wazi kuwa, hata mafundisho toka kwa watumishi wake ni lazima yaendane na Neno la Mungu, Ukiona kiongozi wako, mchungaji, askofu, mwalimu, mwinjilisti, mtume, au nabii wako, anafundisha mafundisho ambayo ni kinyume na Neno la Mungu nakushauri ondoka mapema hapo kwani huyo kiongozi kipofu.
Mpendwa, Kama kiongozi wa kanisa lako anaruhusu wanawake wajipambe kwa kupaka ma lipstick, make up, wanja, kuweka wivin kichwani, kusuka nywele na kusuka kusuka rasta, na tena anakwambia mambo hayo ni sawa Mungu anatazama roho na si mwili, hapo ulipo si mahali salama unapotezwa, neno la Mungu linakutaka uutoe mwili wako dhabihu safi na takatifu kwa Mungu na wala usifuatishe namna ya dunia hii (Fashion).
Warumi 12:1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 WALA MSIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
binti, mama mwili wako ni dhabihu takatifu yaani (sadaka) iliyo hai Hivyo binti, mama, usipotezwe na mafundisho hayo ya kiongozi kipofu kwa kusema Mungu hatazami mwili bali anatazama roho tu, kama Mungu anatazama roho tu kwanini unaenda na mwili kanisani? Si ungeuacha nyumbani, hivyo ni wazi Mungu anatazama vyote, na kusudi la kutupa vyote hivi viwili ni kwamba, vyote vimtukuze Mungu Muumba mbingu na nchi, na siyo kimoja kitende ya ulimwengu huu na kimoja kitende mapenzi ya Mungu huo ni uongo, huwezi kuwa mtakatifu ndani alafu nje kama wakidunia
Yakobo 3:12 Ndugu zangu, Je! Mtini waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? KADHALIKA CHEMCHEMI HAIWEZI KUTOA MAJI NA YA CHUMVI NA MAJI MATAMU.
Kilichomo rohoni mwako ni lazima kidhihirike na nje, yaani utakatifu ndani na nje pia, hivyo toka hapo kwa kiongozi kipofu na ulitii neno la Mungu.
Mwanamke, Kama kiongozi wako anaruhusu wewe mwanamke kuvaa vazi la suluari na kuonekana kuwa ni vazi la heshima, basi fahamu kuwa hapo hapakufai ondoka mapema, vazi la suruali ni vazi la kiume na wala halikusitiri wewe mwanamke badala yake linakuchora maungo yako yote na unakuwa uchukizaye mbele za Bwana.
Kumbukumbu la Torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Hivyo uamuzi upo kwako, kumfuata kiongozi wako au Neno la Mungu.
Kama kiongozi wako anakuhubiria injili ya mafanikio na kukufundisha jinsi ya kupata pesa toka hapo kwani ni kiongozi kipofu, mafundisho kama hayo yanapaswa kuwepo kwenye vyuo vya biashara na kwenye vikundi vya ujasiliamali na sio kanisani, unachopaswa kufanya ni kutoka kwa huyo kiongozi kipofu na kuigeukia injili ya kweli kwa kutubu dhambi zako na kwenda kubatizwa katika ubatizo sahihi, na kuishi maisha ya utakatifu ambao pasipo huo hakuna atakaye Mwona Bwana.
Waebrania 12:14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Shalom.