Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lisifiwe milele na milele….
Karibu tujifunze kwa njia ya ndoto ili tupate maarifa ya kumsikia Mungu kwa njia hiyo
Asilimia kubwa ya ndoto tuotazo huwa zinatokana na harakati na mizunguko mingi ya maisha yetu hususani shughuli zetu za kila siku, lakini ikitokea ndoto yako haijaingiliana na shughuli yoyote au akili zako, imekuja kwa tofauti kidogo, hapo yakupasa kuitafutia maana yake…..
Ukiota unakimbizwa na simba, hiyo ni ishara ya kwanza kuwa Matendo yako hayaendani na kanuni za Mungu na hivyo husababisha ukutane na siku ya hasira ya Bwana
Maandiko yanasema…
Amosi 5:18-20
[18]Ole wenu! Ninyi mnaoitamani siku ya BWANA; kwani kuitamani siku ya BWANA? Ni giza, wala si nuru.
[19]Ni kama mtu aliyemkimbia simba, akakutana na dubu; au aliingia katika nyumba akauegemeza mkono wake ukutani, nyoka akamwuma.
[20]Je! Siku ya BWANA haitakuwa giza, wala si nuru? Naam, yenye giza sana, wala haina mwanga.
Hivyo hakikisha utakatifu ni sehemu ya maisha yako ya kila siku, hakikisha sadaka zako,wokovu wako,nyimbo zako na ibada yako yote inaendana na matendo yako….
Amosi 5:21-23
[21]Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.
[22]Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.
[23]Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaki kuzisikia sauti za vinanda vyenu.
Dumu katika usafi pamoja na kumpendeza Bwana kwa mwenendo wako na tabia yako,hizi ni siku za mwisho Kristo yu mlangoni kuchukua walio wake,utakuwa wapi…..
Shalom….