Kuota unafukuzwa na Mbwa, au umeumwa na Mbwa, au umezungukwa na mbwa
Maana yake nini?.
Mnyama Mbwa katika roho anawakilisha vitu viwili.
1. Roho ya uzinzi/uasherati
2. Roho za manabii wa uongo.
3. Roho ya umaskini.
Katika biblia wanaume wanaofanya kazi ya kujiuza kinyume na maumbile walijulikana kama Mbwa.
Kumbukumbu 23:18 “Usilete ujira wa kahaba, wala mshahara wa mbwa, katika nyumba ya BWANA, Mungu wako, kwa ajili ya nadhiri yo yote; kwani haya ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako, yote mawili”.
Hivyo ukiona unakimbizwa na Mbwa, basi fahamu kuwa aidha kuna roho ya uzinzi inakunyemelea au kukufuatilia.
Lakini kama sio roho ya uzinzi, basi jua ni roho za manabii uongo ambao wanakuja kwa mavazi ya kondoo lakini ndani ni mbwa mwitu wakali.
Mathayo 7:15 “Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali”.
Wafilipi 3:2 “Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao”.
Na mwisho, Mbwa anawakilisha roho ya umaskini, ukiota unalambwa na mbwa, au umezumgukwa na mbwa kama ndio tumaini lako, basi ni ishara kuwa upo katika hali ya umaskini katika roho, au hata katika mwili, (Soma Ayubu 30:1,2Samweli 2:9, 2Wafalme 8:13,2Samweli 16:9, Marko 7:28, luka 16:21) na kama haupo sasa basi unakuja mbele yako, hivyo huna budi kuchukua hatua kuyarekebisha maisha yako..
Je umepata tafsiri ya ndoto yako?
Kama umepata basi shiriki ujumbe huu na wengine.
Na kama umeota Mbwa na bado unahitaji maelezo zaidi, binafsi basi unaweza kutuma ndoto yako kupitia email yetu ya info@ndotozangu.com.
Pia pata nakala yako kitabu cha ndoto mbalimbali kwa njia ya PDF