Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

unapoota ajali

UNAPOOTA AJALI NINI MAANA YAKE?

Posted on February 8, 2022

Mtu anaweza kuota kapata ajali ya pikipiki, au ya gari, wengine wengine ajali za ndege, wengine treni, katika namna tofauti tofauti. Wengine wanaota mtu kagongwa na gari, au magari yanagonga gongana n.k…

Sasa hizi ndoto zinawajia watu wa makundi makuu mawili

1.) Kundi la kwanza ni waliompokea Yesu (yaani waliokoka).

2) Kundi la pili ni wale ambao hawajampokea Yesu.

kundi la kwanza (watu ambao hawajaokoka): kama umeokoka kikamilifu.  Basi kuna uwezekano Mungu anakutahadharisha tukio lililopo mbele yako, aidha kuna ajali inakuja, au itatokea kwa mtu mwingine unayemfahamu,  Hivyo  unachopaswa kufanya, ni kuzama katika maombi ya kina kuharibu hiyo mipango ya adui. ..(Soma Ayubu 33:14-15)

Kundi la Pili: Kwa ambaye hajaokoka.

Ikiwa wewe haujaokoka, yaani Kristo hayupo ndani yako). Ujue ndoto hiyo ni ishara ya tahadhari kubwa sana kwako. Kwamba kipindi si kirefu kuna kuna janga litakupata.

Fuatilia habari hii;

Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.

7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.

8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.

9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.

10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.

Umeona? Ikiwa  wewe ni mzinzi, basi fahamu kuwa kuna ajali ya Ukimwi ipo mbele yako,  ikiwa wewe ni fisadi ajali ya vifungo  inakuja, wewe ni mwizi ajali ya kifo inakuja, wewe ni mshirikina ajali ya ziwa la moto inakuja.

Je bado unasubiri mpaka hayo yakukute? ,Tubu leo na  Yesu atakusamehe, na kukunusuru na hayo yote. Angeweza kukaa kimya tu, hayo mambo yakutokee, lakini kwasababu anakupenda ndio maana anakuonya mapema.. Hivyo mpokee leo na kubatizwa.


KUOTA UNAJENGA NYUMBA

KUOTA MTI UMEANGUKA

KUOTA UNAOKOTA HELA

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz