Kama shughuli yako ni kilimo, basi kuota upo shambani unavuna ni jambo la kawaida, kwasababu maandiko yanasema ndoto huja kutokana na shughuli nyingi.
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi…”.
Lakini kama shughuli zako si kilimo na wala hujawahi kujishughulisha na kilimo, lakini unajikuta unaota upo shambani, unalima au unavuna, shamba lako binafsi au shamba la mwingine.
Basi tafsiri ni kwamba kuna ufalme unaoutumikia katika roho kwa kujua au pasipo kujua, na ufalme huo ni aidha ufalme wa Mungu au ufalme wa giza, inategemea na ndoto hiyo inavyojieleza.
Bwana Yesu alisema..
Mathayo 9:37 “Ndipo alipowaambia wanafunzi wake, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache.
38 Basi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake”.
Umeona hapo?..Wahubirio injili katika roho wanafanya kazi ya kuvuna..
Vile vile wahubirio au watangazao mambo mabaya katika roho ni wavunaji.
Kwahiyo unapoota upo katika kuvuna! Na wewe si mkristo, au kama ni mkristo basi ni mkristo kwa jina tu au vuguvugu!..basi tambua kuwa unautumikia ufalme wa giza na unauletea mazao pasipk wewe kujua.
Na ufalme wa giza mtu anaweza kuutumikia akiwa shuleni, au kazini kwake au katika shughuli yoyote anayoifanya.
Suluhisho la kutoka katika utumishi wa ufalme wa giza ni kutubu dhambi na kumpokea Yesu na kusimama katika wokovu.
Maran atha!