Shalom……
Karibu tujifunze Biblia takatifu ambalo ndilo Neno la Mungu wetu…..
Wengi wetu tumeshawahi kulisikia hili Neno ziwa la Moto na pengine limeshakuwa mazoea kwetu kulitaja,lakini nimependa leo tuliangalie kwa namna nyingine tena naamini kuna mambo utajifunza….
Tukilileta kwa lugha rahisi hili Neno ziwa la Moto tutaitafsiri kama Adhabu,.na tukumbuke Adhabu hi haikutolewa kwa wanadamu bali kwa shetani,na mpaka adhabu hii inatolewa ni kutokana umekiuka maagizo au amri ulizowekewa uzishike….ndivyo tunavyoona kwa shetani
Mathayo 25:41
[41]Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;
Umeona hapo Maandiko yanasema kumbe ziwa la moto au hii adhabu aliwekewa shetani na Malaika zake kwa kuyaasi Maagizo ya Mungu waliyowekewa…
Lakini tunakuja kuona adhabu hii imekuja mpaka kwa Ulimwengu mzima,kwa wale ambao na wao watakiuka sheria za Mungu ziwa hili la moto litawahusu, ndivyo maandiko yanavyotujuza,ina maana kama leo hii aupo katika kitabu cha uzima basi jua wewe upo katika adhabu hii ya milele..
Ufunuo wa Yohana 20:15
[15]Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Hii ni hatari sana
Leo hii unafanya mambo mabaya kwa maamuzi yako na huoni shida yoyote,unazini huoni ukipata magonjwa ndo kwanza unafanikiwa,unafanya uasherati sana ni mlevi wa kupindukia,unasengenya sana ,unaabudu sanamu za Maria na kuzitumikia,unafanya mambo mabovu hata hayajawahi kutokea,wewe unajiona unajiweza kwa kila kitu hakuna anayekupangia chochote,lakini fahamu Neno hili….
Ufunuo wa Yohana 21:8
[8]Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Adhabu yako ilishatangazwa juu yako mda mrefu ni kipindi kinasubiriwa kifike upokee adhabu yako kwsababu ulikiuka Maagizo yake toka ukiwa duniani..
Sasa kwanini hayo yakukute ndugu yangu,Kumbuka adhabu hiyo ni ya milele na milele utateseka na kusumbuka hakuna atakayekuonea huruma kwsababu Mungu ni Mungu wa waliohai siyo waliokufa katika dhambi, hivyo hata siku ya adhabu yako hatasikia maumivu yako kama wewe ambavyo utaki kusikia Maagizo yake leo….
Embu chukua maamuzi leo,saa ya wokovu ni sasa,hizo adhabu zilitangazwa kwa shetani na mapepo yake siyo wewe…Mkabidhi Yesu Kristo maisha yako leo kwa kutubu dhambi zako zote na ubatizwe ubatizo sahihi kwa Jina lake Yesu Kristo ili jina lako liandikwe kwenye uzima wa milele,Maamuzi ni yako…
Yohana 1:12
[12]Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
Shalom..
Washirikishe na wengine habari hizi kwa kushea…