Karibu tujifunze Maneno ya Bwana wetu na Mwokozi wetu Yesu Kristo….Ni kwa neema zake hata tumeiona siku mpya ya tarehe ya leo…
Zipo ngazi nyingi ambazo ukizipanda unaweza kumkaribia Mungu au hata kumuona Kabisa,wakati mwingine unaweza ukawa mtu wa haki,unaweza ukawa una huruma kwa wengine, ni mtu wa kusamehe sana,ni mtu wa kuwajali wengine,uko tayari kujitoa kwa wengine pasipo kuagalia hali yako au hata kipato chako,sasa kikawaida katika ngazi hizi zote na nyingine nyingi lazima kwa namna moja utamwona Bwana katika matendo hayo yote kwsababu Neno linasema Mungu hana upendeleo,ukimtafuta kwa njia yoyote ya haki utamwona tu…
Lakini ipo ngazi au njia ambayo katika hiyo ukiweza kuipanda na kuipita njia hiyo basi utafanana Mungu kabisa,ngazi hiyo si nyingine zaidi ya UPENDO….
1 Wakorintho 13:13
[13]Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
Umeona hapo…sisi wanadamu tunaupendo wakupendana sisi kwa sisi tu na baadhi ya vitu tena si vyote tena tuna machaguzi ya kuchagua vipi tuvipende vipi tuvichukie,kwsababu tumeumbwa kwa taswira ya Mungu mwenyewe kuna vimelea vidogo vya upendo vipo ndani yetu lakini kama isingekuwa hivo,Upendo tungekuwa tunausikia tu,Ndo mana kufikia upendo ule wa KiMungu unahitaji bidii na kujitahidi sana kwsababu ukifikia hu upendo wa Mungu basi hata kuishi kwako ulimwenguni kutakuwa hakuna haja tena….
Lakini kwa Mungu watu ni tofauti kabisa na jinsi alivyotuumba watu wake…Upendo wake ni mkuu sana,upendo wake kwetu haungalii sisi tuna nini,alitupenda hivyo hivyo,Maandiko yanasema kila alichokiumba aliona ni chema,ni kizuri,kinapendeza na amependezwa navyo,,ndo mana leo ukiwa na sababu elfu za kumchukia mtu na kumwona hafai hiyo ni kwako lakini mbele za Mungu anamwona ni mtoto anastahili upendo wote…
Lakini upendo wa Mungu haukuishia tu moyoni mwake bali aliudhihirisha kwa ulimwengu mzima,hapo kwanza tuliuona kwa taifa lake teule Israeli jinsi upendo wa Mungu ulivyowatoa katika mikono ya mateso,mikono ya wamisri kwa uweza na Nguvu nyingi…ndo mana aliwaambia maneno haya..
Kumbukumbu la Torati 7:6-9
[6]Kwa maana wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako; BWANA Mungu wako, amekuchagua kuwa watu wake hasa, zaidi ya mataifa yote walioko juu ya uso wa nchi.[7]BWANA HAKUWAPENDA ninyi, WALA HAKUWACHAGUA NINYI, KWA SABABAU MLIKUWA WENGI KULIKO MATAIFA YOTE, MAANA MLIKUWA WACHACHE KULOKO WATU WOTE;
[8]bali kwa sababu BWANA anawapenda, na kwa sababu alitaka kuutimiza uapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu, akawakomboa katika nyumba ya utumwa, katika mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
[9]Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu;
Umeona hapo ee…Mungu anawaambia Israel si kwsababu mlikuwa wengi kuzidi mataifa yote duniani wala si kwsababu mlikuwa wachache kuliko watu wote,anawaambia hiyo siyo sababu iliyonifanya niuonyeshe upendo wangu kwenu, sababu ni kwamba niliwapenda tu na sababu niliyowapenda zaidi ni ili nitimize uapo ule niliomwapia Ibrahimu baba yenu….Huu ni upendo wa ajabu sana…
Embu tafakari safari yote ya Wana wa Israeli mpaka mwisho uone ni upendo wa aina gani Mungu aliouonyesha kwa watu wake,embu Soma uone jinsi alivyotembea nao kwa upole,kuwabembeleza,kwa huruma na nguzu za ajabu,embu anza up ya kuosma kuanzia kutabu cha Mwanzo,endelea na kutoka,ingia ndani zaidi na Kumbukumbu la torati,zidi kuchimba ndani ya Mambo ya Walawi,Hesabu na Yoshua…embu kaa chini na utafakari uuone huu upendo wa KiMungu jinsi ulivyo mkubwa….
“Sifa kwa Mungu “
Hili pendo la Mungu halikuishia kwa Wana wa Israeli tu…Limekuja kujidhihirisha kwetu sisi watu wa Agano Jipya kwa namna kubwa zaidi ya waIsraeli,sisi kwetu limekuwa ni pendo ambalo hata kulielezea kwa kina huwezi,ni pendo la ajabu sana,ni pendo kuu mno…ndo hili tunalisoma katika Neno la Mungu….
Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Tuna nini cha kusema tena Mbele za Mungu kwa upendo wake mkuu namna hii wa mtu kumtoa mwanawe mpendwa kwa ajili ya wengine,watu wa Agano jipya tuna Upendo wa Mungu unaoitwa Yesu Kristo..huu ni upendo usiochangua chochote,ni pendo linalokupenda pasipo kukuangalia wewe ni nani…
Kwanini usiuthamini huu upendo ndugu yangu,Kwanini usitafakari ukauona huu upendo wa Mungu ndani ya maisha yako…unataka nini tena, jiulize bado unakunywa pombe,bado unavuta sigara ni mzinzi, unasengenya watu,unavaa utupu na unatembea barranco,unafanya mambo yanamchukiza Mungu lakini bado unapumua,bado unaamka salama kila siku,bado Mungu anakupa rizki,anakulinda na ajali na mambo mabaya yasikupate,anahakikisha udhuriki na kitu chochote kibaya mpaka leo hii unaishi salama, embu tafakari umempa nini Mungu,umefanya nini cha ziada kwa Mungu…kwanini wengine wanakufa na kudhurika na mambo mabaya lakini wewe ni mzima….kwanini wengine wapo mahututi hospitalini na wagonjwa wasiojiweza lakini wewe u na afya tele,umelipa nini kwa Yesu Kristo…
Ukitafakari hayo utagundua kumbe hakuna chochote zaidi ya Huu upendo wa Yesu Kristo wa kufa kwa ajili yetu,wa kufa kwa ajili ya nafsi yangu na dhambi zangu….Kwanini usilithamini hili pendo ndugu,
Embu lia na kuomboleza uyasikiapo maneno haya ya Yesu Kristo,Tubu leo kwa kumaanisha kabisa kukaa mbali na dhambi na kulifuta hili pendo la Mungu,maanisha kabisa ndani ya moyo wako na kutafakari ni mangapi Bwana aliyokutendea mpka leo hii ili uwe na sababu za Kumwamini Yesu Kristo Mwokozi wetu…..
Kumbuka hilli pendo halitadumu nawe siku zote kama utakuwa na moyo wa kutokutii…
Wasambazie na wengine pendo hili…
Bwana atusaidie…