Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

KUOTA UNAKIMBIZWA

KUOTA UNAKIMBIZWA

Posted on March 22, 2022October 30, 2022

Ndoto hii ni kutoka kwa Adui shetani, haijalishi kinachokukimbiza ni nini?.. kama ni mtu, mnyama, ndege, nyoka, au chochote kile ni kutoka kwa Yule adui.…

Siku zote kitu kinachokimbizwa ni kitu kilicho dhaifu, cha kuwindwa ili kiliwe, au kiharibiwe,

Kama unaota unakimbizwa na watu waovu, tafsiri yake ni shetani anakutafuta akudhuru au akuue, kama unakimbizwa na polisi, tafsiri yake ni shetani anakutafuta ili akufunge katika vifungo fulani vya kiroho au kimwili, kama unakimbizwa na mnyama tafsiri yake adui anakutafuta ili akumeze au kukudhuru…

Nyumbu anakimbizwa na simba, ni kwasababu ni chakula mbele ya simba na pia ni dhaifu, lakini kitu chenye ujasiri wote kamwe hakiwezi kukimbizwa, bali chenyewe ndio kinakimbiza!.

Ukijiona unakimbizwa moja kwa moja tafsiri yake ni kwamba “upo dhaifu kiroho”, na hiyo  ni kutokana na kuwa upo nje ya Kristo au kama upo basi hauijatambua mamlaka au nafasi uliyona yo ndani ya Kristo kwasababu aidha ya uchanga uchanga wa kiroho au kwa kuzembea kutojibidiisha kwa Mungu.

Mithali 28:1 “Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu; Bali wenye haki ni wajasiri kama simba”.

Hivyo suluhisho hapo ni kuokoka na kusimama kikweli kweli…

Vile vile anza kujifunza biblia kwa bidii, na pia hudhuria kanisani ili ukue katika Neno la Mungu, ina ili Neno likae kwa wingi ndani yako, upate kujua mamlaka uliyonayo katika Kristo. Mpaka ufikie ujasiri wa wewe kuanza kumfukuza shetani na majeshi yake, na si yenyewe kukufukuza wewe.

2Wakorintho 10:4 “(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)”

Maandiko yanasema pia, shetani ni kama simba akitafuta mtu ammeze.. hivyo usipuuzie ndoto kama hizo.. Fanya hima uokoke, na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu, na utapokea kipawa cha Roho mtakatifu baada ya hapo.

Ubarikiwe.


KUOTA UNANYESHEWA NA MVUA

MAANA YA KUOTA UNAFANYA MAPENZI.

KUOTA UNAJENGA NYUMBA.

UNAPOOTA UNAJIFUNGUA MAANA YAKE NINI?

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Millie peter
Millie peter
Guest
1 year ago

be blessed

1
Reply

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz