Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

kuota ng'ombe

Kuota Ng’ombe (Unakimbizwa, umempanda n.k)

Posted on August 9, 2024

Angalizo: Ndoto inaweza kuwa na tafsiri zaidi ya moja, hivyo baada ya kusoma tafsiri hizi, ni vyema ukaketi na kumwuliza Roho Mtakatifu kwa uthibitisho kamili.


Kibiblia Ng’ombe anawakilisha “Mwaka”.  Kama kabla ya kulala ulikuwa huwazi mambo ya Ng’ombe wala kuyatafakari kwa siku hiyo, halafu ukajikuta usiku au mchana umeota Ng’ombe, aidha anakukimbiza, au wewe unamchunga, basi ifuatayo inaweza kuwa tafsiri yake.

Ng’ombe kibiblia anawakilisha “Mwaka”.. akiwa mmoja ni mwaka mmoja, wakiwa wawili ni miaka miwili,…wakiwa saba ni miaka saba n.k

Mwanzo 41:26 “Wale ng’ombe saba wema ni miaka saba; na yale masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.

27 Na wale ng’ombe saba, dhaifu, wabaya, waliopanda baada yao, ni miaka saba; na yale masuke saba matupu yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yatakuwa miaka saba ya njaa”.

Kwahiyo ukiona Ng’ombe anakufukuza basi huenda huo mwaka uliopo, unamisuko suko mingi, au utakuwa na misukosuko mingi..Suluhisho ni kumkaribia Mungu Zaidi na kuomba..

Vile vile ukiona umempanda Ng’ombe na anakimbia sana kwa hatari basi vile vile huo mwaka utakubeba lakini utakuwa na hatari nyingi..

Ukiona unamchunga Ng’ombe vizuri na anatoa maziwa mengi, basi mwaka utakuwa wa neema, au kuna neema ikiwa utadumu katika Imani.

Mbali na hayo, Ng’ombe pia anaweza kuwakilisha roho za mapepo, kutegemea ndoto uliyoota. Kama hujampokea Yesu na umeota Ng’ombe anakufukuza nawe unakimbia sana kwa hofu, huwenda pia upo mikononi mwa ibilisi, na anakuonea katika ulimwengu wa roho.

Hivyo suluhisho ni kutubu na kumkaribisha Bwana YESU maishani mwako.

KUOTA UMEKUFA

KUOTA MOTO UMEWAKA

KUOTA UPO JANGWANI PEKE YAKO

KUOTA UNAKIMBIZWA NA SIMBA

KUOTA MTI UMEANGUKA

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Recent Comments

  1. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  2. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz