Kuna ndoto zinazokuja kutokana na shughuli tunazozifanya za mara kwa mara, biblia inasema hivyo katika kitabu cha Mhubiri
Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno”.
Hivyo kama kazi yako ni upishi, ni kawaida kuota unakula au unalishwa, au kama wewe ni mgonjwa, ni kawaida kuota unalishwa chakula na mtu.
Lakini kama hufanyi shughuli yoyote inayohusiana na kupika, au huna ugonjwa wowote wa kulala na kulishwa, halafu imetokea umeota ndoto unalishwa!, na pengine imekuja Zaidi ya mara mbili, basi lipo jambo la kiroho linaendelea..
Ukiota au ukiona ono unalishwa kitu, tafsiri yake ni kwamba “kuna mambo yanaingizwa kwenye ufahamu yako” ambayo aidha yataathiri Maisha yako kwa sehemu kubwa!.
Katika biblia utaona baadhi ya manabii walilishwa vitabu, kwamfano utaona Nabii Ezekieli alilishwa Gombo (yaani kitabu).. na alipolishwa kile kitabu kinywani kilikuwa kitamu lakini tumboni kichungu..
Ezekieli 3:1 “Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha enenda ukaseme na wana wa Israeli.
2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo.
3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali
4 Akaniambia, Mwanadamu, haya! Waendee wana wa Israeli ukawaambie maneno yangu.”.
Tafsiri ya Gombo Ezekieli alilolishwa, ni Maneno ya Mungu kuwekwa ndani yake, maneno ambayo yatatoka katika kinywa chake ambayo kwake yeye (Ezekieli) yatakuwa ni mazuri.. Lakini kwa wale watakaoyapokea hayatakuwa mazuri..
Hali kadhalika, Yohana aliyeandika kitabu cha Ufunuo, alipewa kitabu ale..
Ufunuo 10:8 “Na sauti ile niliyoisikia kutoka mbinguni ilinena nami tena, ikisema, Enenda, ukakitwae kile kitabu kilichofunguliwa katika mkono wa yule malaika, aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi.
9 Nikamwendea malaika yule nikamwambia kwamba anipe kile kitabu kidogo. Akaniambia, KITWAE, UKILE, NACHO KITAKUTIA UCHUNGU TUMBONI MWAKO, BALI KATIKA KINYWA CHAKO KITAKUWA KITAMU KAMA ASALI.
10 Nikakitwaa kile kitabu kidogo katika mkono wa malaika yule, nikakila; nacho kikawa kitamu kama asali kinywani mwangu, na nilipokwisha kukila tumbo langu likatiwa uchungu.
11 Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi”.
Hivyo ukiona unalishwa kitu, au unapewa kitu ule ni jambo la kuwa makini sana.
Je unacholishwa ni kitu gani? Na anayekulisha ni mtu wa namna gani?
Kama umelishwa vitu na mganga, fahamu kuwa ni mambo mabaya yamepandikizwa katika Maisha yako, hivyo haraka sana tafuta ufumbuzi ikiwemo kumpokea Yesu, na vilevile kusimama, na watafute watumishi wa kweli wa Mungu wakiombee na kukufundisha njia zinazompendeza Mungu, Na sio mganga tu!, bali hata mtu au watu!, na umelishwa vitu visivyoeleweka, au wakati mwingine vinavyoeleweka.. Kemea hiyo ndoto, au watafute watumishi wa kweli wa Mungu wakufundishe njia sahihi ya Bwana.
MAANA YA KUOTA UPO MAKABURINI.
MAANA YA KUOTA UNAFANYA MAPENZI.
Good article. I absolutely love this site.
Stick with it!
Amen amen