Mtu anaweza kuota kapata ajali ya pikipiki, au ya gari, wengine wengine ajali za ndege, wengine treni, katika namna tofauti tofauti. Wengine wanaota mtu kagongwa na gari, au magari yanagonga gongana n.k…
Sasa hizi ndoto zinawajia watu wa makundi makuu mawili
1.) Kundi la kwanza ni waliompokea Yesu (yaani waliokoka).
2) Kundi la pili ni wale ambao hawajampokea Yesu.
kundi la kwanza (watu ambao hawajaokoka): kama umeokoka kikamilifu. Basi kuna uwezekano Mungu anakutahadharisha tukio lililopo mbele yako, aidha kuna ajali inakuja, au itatokea kwa mtu mwingine unayemfahamu, Hivyo unachopaswa kufanya, ni kuzama katika maombi ya kina kuharibu hiyo mipango ya adui. ..(Soma Ayubu 33:14-15)
Kundi la Pili: Kwa ambaye hajaokoka.
Ikiwa wewe haujaokoka, yaani Kristo hayupo ndani yako). Ujue ndoto hiyo ni ishara ya tahadhari kubwa sana kwako. Kwamba kipindi si kirefu kuna kuna janga litakupata.
Fuatilia habari hii;
Ezekieli 7: 6 “Mwisho umekuja, mwisho huu umekuja; unaamka ukupate; angalia, unakuja.
7 AJALI YAKO IMEKUJIA, wewe ukaaye katika nchi hii; majira yamewadia, siku ile inakaribia; siku ya fujo, wala si ya shangwe milimani.
8 BASI HIVI KARIBU NITAMWAGA GHADHABU YANGU JUU YAKO, nitazitimiza hasira zangu juu yako, nami nitakuhukumu sawasawa na njia zako; nami nitakupatiliza machukizo yako yote.
9 Jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma; nitakupatiliza njia zako na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako; nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, napiga.
10 ANGALIA, SIKU HIYO; ANGALIA, INAKUJA; AJALI YAKO IMETOKEA; fimbo imechanua, kiburi kimechipuka”.
Umeona? Ikiwa wewe ni mzinzi, basi fahamu kuwa kuna ajali ya Ukimwi ipo mbele yako, ikiwa wewe ni fisadi ajali ya vifungo inakuja, wewe ni mwizi ajali ya kifo inakuja, wewe ni mshirikina ajali ya ziwa la moto inakuja.
Je bado unasubiri mpaka hayo yakukute? ,Tubu leo na Yesu atakusamehe, na kukunusuru na hayo yote. Angeweza kukaa kimya tu, hayo mambo yakutokee, lakini kwasababu anakupenda ndio maana anakuonya mapema.. Hivyo mpokee leo na kubatizwa.