Kikawaida mtu unapo safiri, huwa unakutana na mandhari nyingi na tofauti tofauti, sehemu nyingine utakutana na mandhari za joto, za mvua, sehemu nyingine utakutana na mazingira ya hatari
Wana wa Israeli walipotolewa katika nchi yao, wakiwa njiani kuelekea Babeli walilia sana, zaidi sana wakaldayo waliwaambia wawaimbie nyimbo za nchini kwao, lakini walishindwa..na hawakuweza, kwa jinsi mioyo yao ilivyokuwa mizito.
Zaburi 137:1 “Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi, Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.
2 Katika miti iliyo katikati yake Tulivitundika vinubi vyetu.
3 Maana huko waliotuchukua mateka Walitaka tuwaimbie; Na waliotuonea walitaka furaha; Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.
4 Tuuimbeje wimbo wa Bwana Katika nchi ya ugeni”?
Walikuwa na huzuni kwasababu walijua kabisa mazingira waliyokuwa wanayaendea yalikuwa mapya tofauti na nchini kwao,
Hivyo unapojiona kwenye ndoto upo katika nchi ya ugenini, unaishi huko, au unatembea, Yapo mambo mawili hapo ambayo Mungu anakuonyesha.
Ikiwa wewe umeokoka, (yaani umempokea Yesu), Hapo ni Mungu anakuonesha wazi jinsi itakavyokuwa pale utakapotoka kwenye uwepo wake. Utakuwa kama mfungwa, na mtumwa asiye na uhuru, hivyo jitathmini na kujichunguza..kama hujampokea Yesu, fanya hima mpokee ili uthibitike.
Lakini ikiwa hujaokoka, ni Bwana anakuonesha hali yako ya kiroho jinsi ilivyo, kwamba haupo nyumbani.. Maandiko yanasema “Mwana hukaa nyumbani siku zote”
Yohana 8.34 “Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambia, Kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Wala mtumwa hakai nyumbani sikuzote; mwana hukaa sikuzote.
36 Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli”.
Hebu jitafakari maisha yako, ni faida gani umepata katika ulevi, au uasherati, au wizi au uuaji.. zaidi ya matatizo tu!, Zingatia leo kurudi nyumbani ili uwe huru!, na nyumbani kwako ni kwa Yesu!, mrudie Yesu uwe salama..tubu dhambi zako uwe safi!, Usiwe kama Kaini ambaye Mungu alimwabia atakuwa mtoro na mtu asiyekuwa na kikao duniani, baada ya kumwua ndugu yake.