1.je! sanduku la agano lilitengenezewa kwa mbao za mti gani?
___________________
2.je katika Israeli ni kabila gani ambalo Mungu aliliondoa katika kitabu cha ufunuo kwa sababu ya uovu wao na kuwapa nafasi hiyo wana wa Yusufu?
______________________
3.Je katika biblia ni nani aliye weka nadhiri ya kuwa akishinda vita ananapo ludi nyumbani wakwanza kumlaki itakuwa sadaka ya Kuteketezwa kwa Bwana na akatoka binti yake?
_________________________
4. A) Je! Ni mfalme gani aliye tawala Israeli kwa muda mchache kuliko wote?
__________________
B)je! ni mfalme gani aliye tawala yuda kwa muda mrefu zaidi kuliko wote?
___________________
5.je YESHURUNI ni nani?
__________________
6. Je! Paulo baada tu ya kuokoka alienda mji gani?
_________________
7.je andiko hili lapatikana wapi katika biblia (mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume)?
__________________
8.je ni mji gani ambako Bwana Yesu aligeuza Maji kuwa divai?
__________________
9. Taja tofauti za imani zinazo watofautisha mafarisayo na masadukayo?
__________________
10.je ni mji gani katika biblia ambao Bwana Mungu aliuteketeza kwa moto?
___________________
Mtihani mwema mjoli wa Bwana.
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618
26/02/2023
MAJIBU YA MTIHANI LEO
MTIHANI WA BIBLIA (PART 10)
(MASWALI YA BIBLIA)
1.je! sanduku la agano lilitengenezewa kwa mbao za mti gani?
Jibu. MTI WA MSHITA
Soma. Kutoka 25:10
___________________
2.je katika Israeli ni kabila gani ambalo Mungu aliliondoa katika kitabu cha ufunuo kwa sababu ya uovu wao na kuwapa nafasi hiyo wana wa Yusufu?
Jibu. Kabila la DANI
Soma .ufunuo 7:4-8
Sababu ya Mungu kuliondoa kabila hilo ni.
==Ndio kabila la kwanza kuleta miungu mingine katika Israeli walipo fika katika nchi ya kaanani.
Soma waamuzi 18:1-31
______________________
3.Je katika biblia ni nani aliye weka nadhiri ya kuwa akishinda vita ananapo ludi nyumbani wakwanza kumlaki itakuwa sadaka ya Kuteketezwa kwa Bwana na akatoka binti yake?
Jibu. YEFTHA
Soma. 11:34-40
_________________________
4. A) Je! Ni mfalme gani aliye tawala Israeli kwa muda mchache kuliko wote?
Jibu. ZIMRI (siku 7)
Soma. 1Wafalme16:9-20
__________________
B)je! ni mfalme gani aliye tawala yuda kwa muda mrefu zaidi kuliko wote?
Jibu. MANASE (miaka 55)
Soma. 2Wafalme 21:1-18
___________________
5.je YESHURUNI ni nani?
Jibu. TAIFA LA ISRAELI
Soma. Isaya 44:1-2
__________________
6. Je! Paulo baada tu ya kuokoka alienda mji gani?
Jibu. ARABUNI
Soma. Wagalatia 1:13-18
_________________
7.je andiko hili lapatikana wapi katika biblia (mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume)?
Jibu. Kumbukumbu la torati 22:5
__________________
8.je ni mji gani ambako Bwana Yesu aligeuza Maji kuwa divai?
Jibu. Kana ya Galilaya
Soma. Yohana 2:1-12
__________________
9. Taja tofauti za imani zinazo watofautisha mafarisayo na masadukayo?
Jibu. Mafarisayo wana amini yote.
Masadukayo
i)Hawa amini ufufuo wa wafu
ii)Hawa amini kuwa kuna malaika
iii) hawa amini roho (roho ya mtu kuishi baada ya kufa, )
Soma. Matendo ya mitume 23:6-8
__________________
10.je ni mji gani katika biblia ambao Bwana Mungu aliuteketeza kwa moto?
Jibu. SODOMA NA GOMORA
Soma. Yuda 1:7
___________________
BWANA YESU awabariki sana.
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618