Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

MAANA YA KUOTA UNAFANYA MAPENZI.

MAANA YA KUOTA UNAFANYA MAPENZI.

Posted on February 11, 2022February 11, 2022

Unapoota  unafanya tendo la ndoa au kuota unafanya mapenzi  ni kiashiria cha nini?

Awali ya yote tunapaswa kufahamu kuwa Ndoto yoyote ya zinaa, haitokani na Mungu..Ni aidha inatokana na mtu mwenyewe au shetani. Leo tutaangazia makundi mawili ya watu wanaoota ndoto za namna hii:

Kama umeota ndoto hii na bado hujaokoka:

Neno la Mungu linasema..

Mhubiri 5:3 “Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;…”

Hii ikiwa na maana kuwa kama shughuli zako za kutwa kuchwa ni kukaa katika mazingira ya vichocheo vya zinaa na basi ni dhahiri kuwa hata utakapolala utakuwa unaota mambo hayo hayo. Kama unafanya kazi Bar, tegemea kabisa ndoto hizo kuziota mara kwa mara, kadhalika wewe ni mzinzi, kuota ndoto za uzinzi itakuwa ni sehemu ya maisha yako, wewe ni mtazamaji wa picha za ngono kwenye mitandao, tegemea kuota ndoto hizo kila siku.. Wewe ni mtu wa kutazama filamu na tamthilia za mapenzi, pamoja na miziki ya kidunia ambayo maudhui yake makubwa ni kuchochea zinaa, tegemea kupata hizo ndoto kila siku. Hivyo unapoota unafanya mapenzi ni kuonesha jinsi gani nafsi yako imeharibiwa na hayo mambo..

Na suluhisho pekee la tatizo hilo ni kumpokea Yesu, kwa dhati kabisa ili ayasafishe maisha yako.

Kundi la Pili ni kwa mtu aliyeokoka.

Ikiwa wewe umeokoka na unaota unafanya mapenzi..basi ni ishara ya kuwa umeanza kupoa kiroho. Ni ishara kuwa maisha yako ya kiroho yanaanza kuwa vuguvugu.. na akili yako imeshaanza kuingiliwa na mawazo ya zinaa.

Ili kutatua tatizo hilo ongeza umakini katika kumtafuta Mungu na kumtumikia, hakikisha huwi na muda ambao upo tu, bila shughuli yoyote, muda wako mwingi tumia kusoma Neno, kuomba, kuhubiri, na muda wako mchache tumia kufanya kazi zako za mikono kama umejaliwa hizo. Kadhalika punguza muda wa kukaa kwenye mitandao na angalia ni wapi ambapo panachochotea tamaa za kimwili, kisha paharibu hapo, vile vile punguza kuzoeana na watu wenye jinsia kinyume na wewe, hata kama ni wapendwa!

Lakini kama umejitazama na kujihakiki kuwa hakuna kulegea kokote wala kupoa kulikoingia ndani ya maisha yako, na umeota hizo ndoto!, basi usipoteze nguvu nyingi kuitilia mkazo hiyo ndoto wala kuitafakari, ikemee kisha songa mbele kana kwamba hujawahi kuota ndoto kama hiyo, kwaufupi upuuzie.

Mwisho ni vyema kujua au kufahamu kuwa moja ya dhambi hatari sana ni dhambi ya zinaa.. Biblia inasema tuikimbie zinaa, sio tuikemee.. Ndoto ya zinaa tunaweza kuikemea, kwasababu pengine ni adui ameituma kwetu, lakini zinaa yenyewe tunapaswa tuikimbie kama Yusufu alivyoikimbia.

1Wakorintho 6:18 “Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu”.


KUOTA UPO MAKABURINI

KUOTA UNAPIGANA NA MTU

KUOTA UNACHIMBA MADINI

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
KUOTA UNAKIMBIZWA - NDOTO ZANGU
3 years ago

[…] MAANA YA KUOTA UNAFANYA MAPENZI. […]

0
Reply

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz