____Maswali ya biblia_____
1.je ni nani mfalme gani aliye ingia katika hekalu la Mungu na kufukiza uvumba kama kuhani Mungu akampiga kwa ukoma?
______________
2. Je. Amri ya tatu inasemaje?
_______________
3.je ni makosa gani ambayo daudi alimkosea Mungu hata,. Mungu akamwadhibu?
________________
4.je wana wa Yusufu wakiume walikuwa wangapi na ni akina nani?
________________
5. Maana ya Shalomu?
________________
6.ni mifupa ya nani iliyo fufua mtu katika biblia?
________________
8.je Bwana Yesu alifanya miujiza ya kuongeza samaki na mikate mara ngapi?
______________
9.je stefano alikufa kwa kifo gani?
______________
10.katika mitume wa Yesu (thenashara) ni wangapi vifo vyao vimerekodiwa katika biblia.
_____________
Bwana Yesu akubariki, shea na kwa wengine.
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618
07/02/2023
___MASAHIHISHO LEO____
MTIHANI WA BIBLIA (PART 19)
(Maswali ya biblia)
1.je ni nani mfalme gani aliye ingia katika hekalu la Mungu na kufukiza uvumba kama kuhani Mungu akampiga kwa ukoma?
Jibu. MFALME UZIA
Soma. 2nyakati 26;16-23
______________
2. Je. Amri ya tatu inasemaje?
Jibu.Kutoka 20:7
Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
_______________
3.je ni makosa gani ambayo daudi alimkosea Mungu hata,. Mungu akamwadhibu?
Jibu. 1)UZINZI NA KUUWA PASIPO HATIA
alizini na mke wa Uria kisha baadaye akamwua Uria katika vita
Soma. 2samweli 11:1-17
2)Aliwahesabu Israeli kwa kutaka kujitumainisha juu ya jeshi lake badala ya Mungu.
Soma. 1Nyakati 21;1-17
________________
4.je wana wa Yusufu wakiume walikuwa wangapi na ni akina nani?
Jibu. Wawili
1)Manase
2)Efraimu
Soma. Mwanzo 41;50-52
________________
5. Maana ya Shalomu?
Jibu. AMANI
Soma. Waamuzi 6;24
________________
6.ni mifupa ya nani iliyo fufua mtu katika biblia?
Jibu. ELISHA
Soma. 2wafalme 13:20-21
________________
8.je Bwana Yesu alifanya miujiza ya kuongeza samaki na mikate mara ngapi?
Jibu. MARA MBILI
1)Aliwalisha makutano kwa hesabu ya wanaume tuu 4000 (bila wanawake watoto kuhesabiwa) Kwa Mikate 7 na visamaki vichache
Soma. Malko 8;3-9
2)Aliwalisha makutano wanaume 5000 (bila hesabu ya wanawake na watoto) kwa mikate 5 na visamaki 2.
Soma. Yohana 6;8-10
______________
9.je stefano alikufa kwa kifo gani?
Jibu. KWA KUPIGWA MAWE
Soma. Matendo ya mitume 7;54-60
______________
10.katika mitume wa Yesu (thenashara) ni wangapi vifo vyao vimerekodiwa katika biblia.
Jibu. WAWILI
1)YUDA. Alijinyonga
soma Mathayo 27:3-5
2)YAKOBO. Alikatwa kichwa na Mfalme Helode.
soma matendo 13;1
_____________
Bwana Yesu akubariki, shea na kwa wengine.
@NURU YA UPENDO
www.wingulamashahidi.org
0652274252 au 0693036618