Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

KUOTA UMEKUFA

Posted on December 30, 2022

Shalom,Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele….

Karibu tujifunze Maneno ya Uzima kwa njia ya ndoto….Kama una ndoto inakutatiza basi usisite kuiandika kwenye box la maoni chini….

Ndoto ya kuota umekufa uwa ina maana nyingi kulingana na ujumbe ambao ulipaswa kufika mahali husika…

Ikiwa umeota ndoto hii na unaona ndani yako una msukumo wa kufahamu maana yake basi ujue kuna jambo Mungu anataka ulifahamu

Ikiwa wewe ni Mke au mume wa mwingine na umekuwa na tabia ya kufanya mambo ya uzinzi na usharati  kwa siri basi fahamu kabisa kifo kipo katikati yako..Kwsababu Biblia inasema katika wanandoa kifo ndio kitakachowatenganisha…

Mwanzo 20:3

[3]Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mkewe mtu.

Kwa kulifahamu hilo yakupasa haraka sana uache mwenendo wako huo mbaya na utubu dhambi zako na uishi maisha Matakatifu…

Ikiwa tabia yako sio hiyo ya kwanza

Basi fahamu kuwa ni maisha yako ya  Kiroho yapo chini sana,huenda umekuwa mtu wa kupenda anasa sana,Mambo ya ulimwengu huu, usiyeweza kujizuia…Hivyo ikiwa ni mtendaji wa mambo hayo hapo unajulishwa umekuwa mfu…

Na suluhisho ni Kumwamini Yesu Kristo na kutubu dhambi zako zote kwa kumaanisha kuziacha na kubatizwa ubatizo sahihi wa maji Mengi na kwa jina lake Yesu Kristo..

1 Timotheo 5:6

[6]Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.

 

Shalom…….

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
watakatifuwasikuzamwisho
watakatifuwasikuzamwisho
Admin
1 year ago

Hakika hiyo ni kweli kabisa

0
Reply
janeth kessy
janeth kessy
Guest
1 year ago

Shalom Mimi nimeota bado nipo hai lakini nyumbani wanasema Mimi nimekufa na wamefanya msiba,baada ya muda nilipopiga simu kuuliza hivo wananiambia niendelee na mambo yangu na watu wasijue uwepo wangu. Hii inamaana Gani?

0
Reply
watakatifuwasikuzamwisho
watakatifuwasikuzamwisho
Admin
Reply to  janeth kessy
1 year ago

Hapo ingia kwenye maombi kwani huenda kuna sumu adui anaiweka kati ya ndugu zako..

0
Reply

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz