Zaburi 65:4-13
[4]Heri mtu yule umchaguaye,
Na kumkaribisha akae nyuani mwako.
Na tushibe wema wa nyumba yako,
Patakatifu pa hekalu lako.[5]Kwa mambo ya kutisha utatujibu,
Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.
Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,
Na la bahari iliyo mbali sana,[6]Milima waiweka imara kwa nguvu zako,
Huku ukijifunga uweza kama mshipi.[7]Wautuliza uvumi wa bahari,
Uvumi wa mawimbi yake,
Na ghasia ya mataifa;[8]Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
[9]Umeijilia nchi na kuisitawisha,
Umeitajirisha sana;
Mto wa Mungu umejaa maji;
Wawaruzuku watu nafaka
Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.[10]Matuta yake wayajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Waibariki mimea yake.[11]Umeuvika mwaka taji ya wema wako;
Mapito yako yadondoza unono.[12]Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vyajifunga furaha.[13]Na malisho yamevikwa kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia, naam, yanaimba.