Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

SIFA NI ZAKO BWANA

Posted on December 26, 2022

Zaburi 65:4-13

[4]Heri mtu yule umchaguaye,
Na kumkaribisha akae nyuani mwako.
Na tushibe wema wa nyumba yako,
Patakatifu pa hekalu lako.

[5]Kwa mambo ya kutisha utatujibu,
Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu.
Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia,
Na la bahari iliyo mbali sana,

[6]Milima waiweka imara kwa nguvu zako,
Huku ukijifunga uweza kama mshipi.

[7]Wautuliza uvumi wa bahari,
Uvumi wa mawimbi yake,
Na ghasia ya mataifa;

[8]Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.

[9]Umeijilia nchi na kuisitawisha,
Umeitajirisha sana;
Mto wa Mungu umejaa maji;
Wawaruzuku watu nafaka
Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.

[10]Matuta yake wayajaza maji;
Wapasawazisha palipoinuka,
Wailainisha nchi kwa manyunyu;
Waibariki mimea yake.

[11]Umeuvika mwaka taji ya wema wako;
Mapito yako yadondoza unono.

[12]Huyadondokea malisho ya nyikani,
Na vilima vyajifunga furaha.

[13]Na malisho yamevikwa kondoo,
Na mabonde yamepambwa nafaka,
Yanashangilia, naam, yanaimba.

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz