Menu
NDOTO ZANGU
  • Home
  • Orodha ya Ndoto
  • Quizzes & Surveys
  • Contant
  • English Articles
  • Kuhusu
  • MASOMO KWA WANAWAKE
NDOTO ZANGU

Je kuna umuhimu wowote wa kukemea makosa hadharani?

Posted on December 6, 2022December 6, 2022

 

Jina la Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe! Karibu tujifunze neno la Mungu wetu..

Kwa Neema za Bwana huu utakuwa ni mwendelezo wetu wa kujifunza Biblia kwa njia ya Maswali na Majibu,hivyo tunakukaribisha sana…

●SWALI

Je ni sahihi kukemea makosa mbele ya watu wengi?

●JIBU

Embu tusome kwanza katika Maandiko Matakatifu tuone yanasemaje….

1 Timotheo 5:20
[20]Wale wadumuo kutenda dhambi uwakemee mbele ya wote, ili na wengine waogope.

Kiuhalisia wa maisha yetu tukimuona mtu anakemea kosa la mwingine mbele za watu ni rahisi kusema anamkosea  heshima Yule mwenye makosa, pengine tungependa amguse au  amuite pembeni ili amkanye Kwa faragha (private)  na mtu mwingine asijue nini kinachoendelea,,kweli ni hekima nzuri sana mana itasaidia  kutokuleta mzozo au fitina,chuki,Malumbano yoyote yasiyokuwa na maana…pia wakati mwingine linakuwa ni jambo La heshima na busara sana…..

Lakini Biblia,inatufundisha kitu kingine tena kikubwa,,,,Kuna wakati inafika inakubidi ukemee hadharani kabisa tena pasipo kuogopa kitu….Hapo ni Mtume Paulo anampa maagizo timotheo,anamwambia wale waliodumu katika kutenda mabaya na dhambi,maana yake ni wakomavu katika kutenda dhambi zao,hawajataka kusikia toka waliovyoonywa,hawakutaka kubadilika na kuacha uovu wao maadam wanajua fikra wakitendacho ni kibaya mbele za Mungu….

Sasa kwa kiwango kama hicho walichokifikia Biblia inasema Kemea hadharani….Kanisa la Kristo limekuwa kama pango la wangang’anyi,Mwanamke anakuja kanisa kama atakavyo,anaingia kanisani na vimini,mwanamke anaingia kanisani na mawigi,amepaka lipstic na mawanja,kwa hali kama hi wewe Mchungaji,Kiongozi wa kanisa kwanini usikemee hadharani,,hao shingo zao wameshazifanya kuwa nzito,Ukiwakemea mbele ya kanisa,mbele ya jamii,mbele za Watu wengi Maandiko yanasema hutawaponya wao tu bali na wengine pia wataogopa ili wasitende dhambi….

2 Timotheo 4:2
[2]lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

Tunaona mfano mzuri Kwa mtume Paulo, yeye katika barua zake zote  hakuficha majina ya watendao maovu  na wale watendao wema, aliwakanya waovu na kuwakemea na wengine kuwataja hadharani pamoja na dhambi zao walizozitenda hadharani… na kuwasifia wema hadharani ambao Hadi Leo hii Bwana ameruhusu  tuwasome katika Neno lake…..

 

2 Timotheo 1:15-16

[15]Waijua habari hii, ya kuwa wote walio wa Asia waliniepuka, ambao miongoni mwao wamo Figelo na Hermogene. 

 

[16]Bwana awape rehema wale walio wa mlango wake Onesiforo; maana mara nyingi aliniburudisha, wala hakuuonea haya mnyororo wangu;

 

2 Timotheo 4:14

[14]Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake.

 

Kiongozi wa Kanisa,Mchungaji,Mtumishi uliyesimama kufanya kazi ya Bwana…Usipalilie uovu na dhambi ndani ya Nyumba ya Mungu,umeshaona kabisa ni watu wasiotaka kubadilika yakupasa uchukue hatua nyingine ya ziada…Ulevi usionekane ndani ya Kanisa,Uzinzi hata usitajwe kwenu,Chuki,visasi na magomvi yakemee,Msimamishe mmoja baada ya mwingine ukiwakemea na kwaonya mbele za Kanisa,ikawe dawa kwao yakuepukana na Mambo hayo maovu na ukaliponye Kanisa la Kristo……….

 

Usiogope kufanya hivyo

Neno hili lawafaa wazazi na walezi wote wa watoto…Ikiwa Mtoto wako yupo katika makundi ya kucheza na wenzake na ukaona kabisa kakosea katikati yao,ni vema ukamkanya hapohapo kwa pamoja,usisubiri afike nyumbani, na ikiwa amestaili kuchapwa basi mwadhibu wakati huohuo ili na wao waogope kutenda kosa hilo,kwa kitendo kidogo tu kama hicho utakuwa umeokoa roho nyingi za watoto mahali hapo….

 Mithali 22:15-

Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali.

 

Na Kwa zile tabia njema, mtoto apongezwe hadharani pia ili na wenzie wapate kujifunza

Bwana atusaidie kulipokea neno lake hili ili tukaziokoe roho nyingi za watu…

Shalom…Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea…..

2 thoughts on “Je kuna umuhimu wowote wa kukemea makosa hadharani?”

  1. Dorcas says:
    December 6, 2022 at 2:56 pm

    Be blessed. Glory to Jesus
    With the power of holy spirit in you may you continue deliver good word of God .

    Amina sana sana mpendwa

    Reply
    1. Magdalena says:
      December 9, 2022 at 5:46 am

      Utukufu kwa Bwana Yesu mpendwa

      Reply

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts

  • BWANA AKALIZIDISHA KANISA KWA WALE WALIOKUWA WAKIOKOLEWA
  • TAFAKARI KWAKO MKRISTO.
  • ZIWA LA MOTO
  • TOKA KWA VIONGOZI VIPOFU.
  • KUOTA UMEKUFA

Recent Comments

  1. Magdalena on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  2. Goodluck on SITIRI MWILI WAKO, USIWE CHANZO CHA MWENGINE KUTAMANI
  3. Goodluck on KUOTA UNAIBIWA SIMU AU UNANYANG’ANYWA
  4. Magdalena on USIMNAJISI BINTI YAKO, ILI KUMFANYA AWE KAHABA.
  5. watakatifuwasikuzamwisho on Je! Ni wanawake gani wanazungumziwa katika (Zaburi 68:11)?

Archives

  • January 2023
  • December 2022
  • November 2022
  • October 2022
  • September 2022
  • August 2022
  • June 2022
  • May 2022
  • April 2022
  • March 2022
  • February 2022
  • December 2021
  • November 2021

Categories

  • Ndoto kutoka kwa Mungu.
  • Ndoto za Adui (shetani)
  • Ndoto za tahadhari.
  • Uncategorized
  • Wanawake

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2023 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress