Nakusalimu katika Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo,Jina lipitalo majina yote,Jina lenye uweza na nguvu….
Karibia tujifunze Maneno ya Uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo..Ni furaha kwa Bwana kila siku tuwe ni watu wa kuongeza maarifa ya Neno lake”
Leo kwa Neema zake tutaangazia tabia moja wapo ambayo walikuwa nayo wanawake waliotutangalia ili na sisi tuwe mfano uleule na wakuzidi katika wokovu wetu…
Biblia inasema..
1 Wakorintho 10:11
[11]Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili kutuonya sisi, tuliofikiliwa na miisho ya zamani.
Kwa namna hiyo basi tunazo sababu zote za kujifunza sana sana Neno la Mungu……
Kuna mambo katika ukristo yanaweza kuonekana ni madogo sana yakitendeka,, lakini hayohayo madogo yakawa na matokeo makubwa sana na likawa jambo lililompendeza Mungu sana tofauti na ilivyodhaniwa..
Embu tafakari kile kitendo cha yule mwanamke aliyempaka Bwana marhamu kichwani..kwake labda lilikuwa kama wazo tu,Kwamba labda naweza kufanya hivi,au nifanye tu kwasababu nampenda Yesu,au nimeona Yesu ajapaka mafuta muda mrefu …Na Biblia inasema marhamu ile ilikuwa ni ya thamani sana….
Lakini tunaona kitendo kile Bwana akikuchukulia kwa urahisi…kilifika kwake kama upendo wa dhati,kilifika kwake kama heshima na kujali,na mwishowe tunaona Bwana akimueshimisha kwa jambo dogo kama hilo la kumpaka mafuta…
Marko 14:3,5-6,8-9
[3]
Naye alipokuwapo Bethania, nyumbani mwa Simoni mkoma, ameketi chakulani, alikuja mwanamke mwenye kibweta cha marhamu ya nardo safi ya thamani nyingi; akakivunja kibweta akaimimina kichwani pake.[5]Maana marhamu hii ingaliweza kuuzwa kwa dinari mia tatu na kuzidi, wakapewa maskini. Wakamnung’unikia sana yule mwanamke.
[6]Yesu akasema, Mwacheni; mbona mnamtaabisha? Amenitendea kazi njema;
[8]Ametenda alivyoweza; ametangulia kuupaka mwili wangu marhamu kwa ajili ya maziko.
[9]Amin, nawaambia, Kila ihubiriwapo Injili katika ulimwengu wote, na hili alilotenda huyu litatajwa kwa kumbukumbu lake.
Mpaka leo vizazi na vizazi tunajifunza na kurejea katika Biblia kuongeza maarifa katika tendo alilolitenda huyu mwanamke…
Embu tuliangazie Jambo lingine ambalo ni dogo lakini lina matokeo makubwa sana katika Ukristo
Tulisome…
Luka 1:39,41
[39]Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
[41]Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
● KUTEMBELEANA
Hili linaweza likawa ni jambo dogo sana katika safari ya wokovu lakini lakini likichukuliwa kwa uzito lina matokeo makubwa sana…
Ukisoma hiyo habari unaona ni Mariamu alivyopata habari za utumishi atakaoufanya na utumishi wa Elisabeti kwa upande wake…lakini tunaona hakurizika tu na kile kitendo cha malaika kumpasha habari za mambo ya Elizabeti,angeweza kusema ahaa nimeshajua kila kitu kuhusu yeye,sina haja nae tena,au angesema ya nini nijisumbue zaidi…tunaona baada ya yule malaika kuondoka jambo la kwanza la Mariamu alilolifanya ni kufunga safari ya kumtembelea Elisabeti……….
Luka 1:39
[39]Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
Kwa kitendo hicho kidogo lakini kilimpa furaha sana Elisabeti na kumfanya ajae zaidi nguvu za Mungu na uthihirisho wa alichokibeba tumboni…..
Mwanamke tabia hii ipo ndani yako? una muda wa kuwatembelea wanawake wenzako,,umejitengea muda wa kuwatembelea hata wale uliowahubiria habari za Yesu,Kama tabia hi haipo katika ukristo wako Yakupasa Ubadilike sasa…
Maandiko yanasema…
1 Petro 4:9
[9]Mkaribishane ninyi kwa ninyi, pasipo kunung’unika;
(Soma tena, wfeso 4:32,wrumi 15:7)
Kitendo cha kumtembeleaa Binti mwenzako au mshirika wa jinsia yako inaleta matokeo makubwa sana kwa yule uliyemtembelea na kwako pia…yawezekana kuna changamoto alizokuwa anapitia zilizomfanya aone hata ukristo ni mgumu lakini kwenda kwako kila wakati kukamfanya ajisikie nguvu nyingi rohoni za kuendelea na wokovu…
Jenga utaratibu wako wa kuwatembelea wale ulokwisha kuwahubiria habari za Yesu Kristo…Yawezekawa injili ulowapa hawakukuelewa vizuri siku moja…endelea na injili nyingine ya kuwatembelea kila muda,ongezea nyama katika hilo…usione unafanya kazi ya kuchosha ukubwa wake utauona mbele usipozimia moyo…Kuna wakati mitume hawakuwa wanamwelewa Bwana lakini walienda nae mpaka mwisho na sasa ndio Mababa zetu wa imani…
Zidisha upendo huo wa kutembeleana…hujui unaongeza kitu gani juu yako na yule unayemtembelea…unaweza usione matunda haraka lakini utayona ukifanya kwa uaminifu…kila kazi inakuwa na mshahara…na wewe pia utavuna roho nyingi kwa Kristo kwa kitendo hicho cha kutembelea…
Anza kuivuta tabia hi ili iwe ndo tabia yako kama mwanamke……
“Tujiweke tayari kwa Mwendelezo wa pili”
Sambaza kwa wengine ujumbe hu kwa kushea….