Fundisho maalumu kwa mwanamke
Kuvaa suruali kwa mwanamke wa Kikristo ni dhambi mbele za Mungu na si sawa hata kidogo, kwa sababu biblia imesema ni mchukizo kwa Bwana Mungu wako, haijalishi wewe ni nani, una cheo gani au wadhifa gani ni machukizo mbele za Mungu.
Kumbukumbu La Torati 22:5 Mwanamke asivae mavazi YAMPASAYO mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni MACHUKIZO KWA BWANA, MUNGU WAKO.
Na biblia inasema, wachukizao wote, sehemu yao ni katika ziwa la moto, haijalishi wadhifa wako ulionao katika jamii wala cheo chako ulichonacho, kama hutotubu na kuanza kuvaa mwanamke, wewe ni miongoni mwa wachukizao.
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na WACHUKIZAO, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Vazi la suruali sio vazi linalompasa mwanamke hata kidogo, kwa sababu vazi hilo lenyewe lipo kulingana na maumbile ya jinsia ya kiume.
Mfano; utaona suruali inayo zipu, ambayo inatoa nafasi ya urahisi kwa mtu wa jinsia ya kiume katika haja ndogo, sasa mwanamke hiyo zipu hapo kwenye hiyo suruali yako ni kwa ajili ya kukupa urahisi katika haja ndogo?..Huoni kama hilo vazi halikupasi kulingana na maumbile yako ya jinsia ya kike?..Vazi linalokupasa mwanamke, au linaloendana na maumbile yako ya jinsia ya kike ni gauni au sketi, ambayo pia inakupa urahisi hata katika haja ndogo kulingana na jinsia yako.
Mwanamke, unatakiwa kufahamu kuwa, sababu ya wewe kuvaa nguo ni ili kusitiri maungo ya mwili wako wote pamoja na sehemu zako za siri, lakini unapovaa suruali tambua kuwa, haisitili mwili wako bali sehemu zako za siri tu, kwa sababu suruali inakuchora maumbile au shepu ya ya mwili wako, inakuchora hips zako, makalio yako, na mwili wako wote kwa ujumla kitu ambacho kinachosababisha wanaokutazama wakutamani na kuzini na wewe mioyoni mwao.
Mwanamke wa Kikristo, unapaswa kuvaa nguo zinazositiri mwili wako wate kwa pamoja na sio suruali, hilo ni moja wapo la vazi la kikahaba.
1 Timotheo 2:9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa MAVAZI YA KUJISITIRI, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama IWAPASAVYO WANAWAKE WANAOUKIRI UCHAJI WA MUNGU.
Hivyo, mama/dada/binti wa Kikristo unayeukiri uchaji wa Mungu, nenda kachome moto hizo suruali zote na anza kuvaa nguo safi zinazoendana na maumbuile yako na zinazositiri mwili wako.
Tafadhari washirikishe na wanawake wengine ujumbe huu.
Shalom.