Menu
NDOTO ZANGU
  • ORODHA YA NDOTO
  • MASOMO YA WANAWAKE
  • QUIZZES/ MITIHANI YA BIBLIA
NDOTO ZANGU

MAANA YA KUOTA UNACHIMBUA VIAZI

MAANA YA KUOTA UNACHIMBUA VIAZI, MIHOGO AU MADINI

Posted on February 8, 2022February 8, 2022

Kama unajihusisha sana na shughuli za mashambani au bustanini ni kawaida kuota ndoto za namna hiyo, kwasababu si kila ndoto tunazoota zinatoka kwa Mungu au shetani, nyingi zinatengenezwa na miili yetu, kutokana na shughuli tunazozifanya mara kwa mara soma  Mhubiri 5:3,

Hivyo kama upo katika mazingira hayo, hiyo ni ndoto ya kawaida tu!, ipuuzie kwasababu ndio shughuli unazozifanya kila siku.

Lakini kama imekujia kwa uzito fulani ambao sio wa kawaida, na huwa huna desturi wala mazoea ya kufanya shughuli hizo basi hilo ni jambo lingine la kiroho… kuna uwezekano kuna riziki inakuja mbele yako

Biblia inasema.

Ayubu 28:5 “Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; …”.

Kama unaishi maisha ya kumpendeza Mungu, yaani umeokoka, basi tegemea jambo zuri mbele yako. Cha muhimu kuliko vyote ni kuzidisha haki yako, ili baraka zako hizo zisipeperuke na kwenda zake..

Unaweza kupitia kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28 yote, usome baraka zote ambazo Mungu kawaahidia wote wamchao.

Lakini kama hujaokoka na ndoto ya namna hii imekujia, ni aidha Mungu anakuonesha baraka utakazozipata endapo utakubali kumpa yeye maisha yako. Kwasababu yeye anatamani wewe ufanikiwe kuliko hata wewe ulivyokuwa na hamu hiyo.


KUOTA UPO NCHI NYINGINE

KUOTA BWANA KARUDI NA UMEACHWA

KUOTA MBWA

PDF
Subscribe
Login
Notify of
guest

guest

0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments

Recent Comments

  1. Lillie on MASWALI YA KITABU CHA 1 WAFALME, I
  2. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  3. Noel Swai on MASWALI, INJILI YA MATHAYO
  4. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA YOSHUA I
  5. watakatifuwasikuzamwisho on MASWALI YA KITABU CHA MWANZO

Palipo na Roho wa Bwana hapo ndipo penye uhuru
©2025 NDOTO ZANGU | Powered by SuperbThemes & WordPress
wpDiscuz