Kama unajihusisha sana na shughuli za mashambani au bustanini ni kawaida kuota ndoto za namna hiyo, kwasababu si kila ndoto tunazoota zinatoka kwa Mungu au shetani, nyingi zinatengenezwa na miili yetu, kutokana na shughuli tunazozifanya mara kwa mara soma Mhubiri 5:3,
Hivyo kama upo katika mazingira hayo, hiyo ni ndoto ya kawaida tu!, ipuuzie kwasababu ndio shughuli unazozifanya kila siku.
Lakini kama imekujia kwa uzito fulani ambao sio wa kawaida, na huwa huna desturi wala mazoea ya kufanya shughuli hizo basi hilo ni jambo lingine la kiroho… kuna uwezekano kuna riziki inakuja mbele yako
Biblia inasema.
Ayubu 28:5 “Katika ardhi ndimo kitokeamo chakula; …”.
Kama unaishi maisha ya kumpendeza Mungu, yaani umeokoka, basi tegemea jambo zuri mbele yako. Cha muhimu kuliko vyote ni kuzidisha haki yako, ili baraka zako hizo zisipeperuke na kwenda zake..
Unaweza kupitia kitabu cha Kumbukumbu la Torati 28 yote, usome baraka zote ambazo Mungu kawaahidia wote wamchao.
Lakini kama hujaokoka na ndoto ya namna hii imekujia, ni aidha Mungu anakuonesha baraka utakazozipata endapo utakubali kumpa yeye maisha yako. Kwasababu yeye anatamani wewe ufanikiwe kuliko hata wewe ulivyokuwa na hamu hiyo.