Shalom.
Mtu apitaye cheo ni mtu wa namna gani?
turejee..
2Yohana 1:9 “KILA APITAYE CHEO, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia”.
Cheo ni kipimo..
Mfano mtu mwenye cheo/nafasi kubwa katika kazi Fulani basi ana cheo kikubwa katika kazi hiyo, au Mtu mwenye nafasi kubwa Serikalini kuliko wenzake tunasema kuwa ana cheo kikubwa..
Marko 6:21 “Hata ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya”
Au tuchukulie mantiki ya kiumri; mwenye umri mkubwa zaidi ana cheo zaidi..
Mwanzo 43:33 “Wakaketi mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa cheo cha kuzaliwa kwake, na mdogo kwa udogo wake; watu hao wakastaajabu wao kwa wao”.
Sasa Je? Mtu apitaye CHEO ni mtu Gani?
Kulingana na muktadha wa andiko hilo ni “avukaye kipimo au mipaka ya mafundisho ya Yesu Kristo”
Au kwa lugha rahisi zaidi ni yule anayehalalisha dhambi
Mfano imeagizwa USIZINI, usiibe; Yeye anatafuta namna ya kuhalalisha dhambi hiyo ingali moyoni mwake anajua wazi kabisa kuwa ni chukizo na imekatazwa! Lakini sababu tu anaitamani anaihalalisha.
Hivyo tunapaswa kudumu na kuliishi neno la Mungu kwa maana Limehakikishwa! Hakuna anayeweza kulirekebisha..
Mithali 30:5 “Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
6 Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo”.
Tena hukumu ya dhambi hiyo ya KUPITA cheo Cha mafundisho ya Kristo inatajwa katika ufunuo 22:18
Ufunuo 22:18 “Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki”.
Bwana Atusaidie tusivuke cheo, Bali tukifikie (Waefeso 4:13)
Ubarikiwe sana
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea.