Jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo libarikiwe milele….Ni siku nyingine kwa Neema zake…
Karibu tujifunze Maneno yake…
….Leo nataka tuitafakari kauli moja ya Mtume Petro,kupitia kauli hiyo tutapata vingi vya kujifunza na sisi..Kama tunavyofamfahamu,ni Mtume aliyekuwa na ufunuo mwingi kumuhusu Yesu,kipindi cha Bwana yupo duniani hata wakati hayupo,alifanikiwa kuzijua siri nyingi sana za Ufalme wa Mungu,na kufikia kupewa ufunuo mkubwa ambao wengi walishindwa kuutambua ya kuwa Yesu Kristo ni mwana wa Mungu…
Mathayo 16:16-18
[16]Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
[17]Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
[18]Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Lakini hatutaingia ndani huko zaidi ila nataka tuione kauli ambayo nilitamani tujifunze zaidi..na tunaisoma hapa….
Luka 5:5
[5]Simoni akajibu akamwambia, Bwana mkubwa, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.
Tunaona hapa ni baada ya Bwana Yesu kukitumia chombo cha Petro kwa muda mrefu kwa ajili ya kuwafundisha makutano,na baada ya Bwana kumaliza ndipo anamwambia Petro tweka mpaka vilindini ukavue samaki,kidogo’kauli hii ilimshtua Petro kulingana na tukio lililowatokea jana kwsababu walifanya kazi usiku kucha lakini hawakuambulia chochote….Lakini tunaona Mtume Petro hakutaka kuwa mbishi ijapokuwa hakuwa anamfahamu Bwana Yesu kwa undani….
Halikuwa jambo rahisi kwa Petro kama tunavyodhania…na wengi tunafahamu shughuli za uvuvi jinsi zilivo ngumu na zenye kujitoa muhanga,lakini tunaona kilichokwenda kumsaidia Petro na kuchukua maamuzi ya haraka NI NENO LA BWANA,ijapokuwa alikuwa hamjui Bwana vizuri,ijapokuwa alikuwa ni mtu mwenye dhambi, hakujalisha ni mambo gani yaliyotupata siku zilizopita ,hakuangalia ugumu uliopo mbele yao tena, KWA NENO LA YESU likampa yeye ujasiri na kuzishusha nyavu,mwisho tunajua ni nini kilichokwenda kutokea….
Ni nini nataka tujifunze
Wengi wa watu wa leo wamebeba nyavu zao na kuzishikilia bila kujua msingi mkuu ni NENO LA MUNGU,wengi nyavu zao ni maarifa waliyoanayo,wengi ni ujuzi wao,baadhi ya wengi nyavu zao ni tamaduni za kwao, mila za kwao,wengine wali wengi nyavu zao ni viongozi wao wa dini…..
NENO LA MUNGU linaposema mwanamke avae mavazi ya kujisitiri,siyo kwa mapambo wala hareni,make up,bangili wala mavazi ya kuuacha mwili wake wazi,
1 Timotheo 2:9
[9]Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
Neno la Mungu linapokuambia hayo usiwe mbishi wewe shusha nyavu zako,shusha chini ujuzi wako,shusha chini uelewa wako,shusha chini nyavu zako zinazokuambia Mungu anaangalia roho sio mwili,weka mbali fikra zako kwamba Mungu ni wa neema hawezi kutuhukumu kwa mavazi shusha chini,kataa mafundisho yanayokuambia wee njo kanisani kama utakavyo,ukiwa umevaa suruali,ukiwa umevaa vikaushi,ukiwa umejipodoa kama nyumba,ukiwa umevaa mawigi,hizo ni nyavu tu haziwezi kukusaidia chochote zishushe ulitii Neno la Mungu linalosema…
1 Petro 3:3-4
[3]Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;
[4]bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.
NENO LA MUNGU linaposema ubatizo sahihi ni wa maji mengi na Kwa jina la Yesu Kristo,usianze kuhojihoji kwa kubisha,wewe shusha nyavu zako chini ukabatizwe, Ndivyo Biblia inavyotufundisha kwamba yakupasa utubu dhambi zako, na kila aaminiye ni lazima abatizwe…..
Matendo ya Mitume 2:38
[38]Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Usianze kulipindua neno kwa itikadi zako unazozifahamu’ shusha chini nyavu hizo,wengi ukiwaambia ubatizo wanakujibu hauna maana sana kwsababu tulishaamini moyoni,hizo itikadi zako inabidi uzishushe chini ulisikilize Neno la Mungu,yapo madhehebu yanaamisha ubatizo hata kwa maji machache,hizo ni nyavu potovu lazima uzikatae kuzitumia…maandiko yanasema
Yohana 3:23
[23]Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.
Mkatae huyo kiongozi wako anayekuamisha ubatizo wa maji machache,zikatae nyavu zinazokuambia ubatizo ni kwa jina baba na mwana na Roho Mtakatifu,hayo ni mafundisho mapotofu,wamekosa ufunuo,yakatae kwa kubatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo sawa na Neno la Mungu,(matendo 2:38)
NENO LA MUNGU linaposema mwanamke hana ruhusa ya kufundisha wala kumtawala mwanaume bali awe katika utulivu lazima ulitii…
1 Timotheo 2:11-12
[11]Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
Wanawake wengi leo wameshikilia nyavu zao za ujuzi kwamba haki sawa kwa wote, hizo ni nyavu bandia zishushe chini hazitakusaidia chochote,wewe unajua haki kuliko aliyekuumba,alipenda kuweka utaratibu wake katika kanisa,wewe ni nani umpangie,nyavu zinazokuambia hata mwanamke anaweza kuwa kiongozi kwenye kanisa zikatae na uzishushe chini, hizo elimu za thiolojia zinazokuamisha baada ya muda fulani ukafungue kanisa zishushe chini,huna mamlaka ya kumtawala mwanaume wewe,…
1 Wakorintho 11:3
[3]Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.
NENO LA MUNGU linaposema mwanamke haruhusiwi kufanya ibada au kwenda kanisani pasipo kufunika kichwa chake lazima ulisikilize hilo neno ….
1 Wakorintho 11:4-6
[5]Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa.
[6]Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Usianze kuziweka sababu zako na kuziona ni za msingi sana,Petro alikuwa na sababu kubwa za yeye kutomsikiliza Bwana lakini aliziweka chini sababu zake akalitii Neno la Mungu,hizo sababu zinazokuambia unaweza kuingia kanisani kama utakavyo,zishushe chini, viongozi wako hawakufundishi wala kukusisitiza wewe kufunika kichwa ila Neno la Mungu linakuambia funika kichwa chako wewe dada,mama..shusha chini nyavu za utaonekanaje kama mbibi,zikatae nyavu zinazokuambia uingie ibadani huku umenyoa mitindo ya kidunia,litii neno la Mungu…
1 Wakorintho 11:10
[10]Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
Lazima tujue msingi mkuu kwa wanadamu wote ni NENO LA MUNGU,pasipo huo usijisifu kwa chochote..
Zaburi 119:140
[140]Neno lako limesafika sana,
Kwa hiyo mtumishi wako amelipenda.
Shalom..
Washirikishe wengine habari hizi njema kwa kushea…