Utukufu na heshima na mamlaka na zivume kwake Bwana wetu Yesu Kristo milele na milele….
Karibu tujifunze kwa njia ya ndoto…Kama una ndoto yako unayohisi inahitaji ufumbuzi wa Kimaandiko basi usisite kuiandika kwenye comment….
Sisi wanadamu kifaa ambacho kimekuwa na umuhimu sana katika ulimwengu wa sasa ni Simu,na kimekuwa cha muhimu kwsababu kina uwezo wa kutoa taarifa moja kwenda sehemu nyingine kwa urahisi…kimeweza kutupa Mawasiliano ya haraka sana
Sasa ikiwa ndoto hi ya kuibiwa simu au unaota unanyanganywa simu na watu unaowajua au usiowajua na inakuja kwako kwa uzito kidogo basi lipo jambo la kuzingatia sana…
Kipindi cha Adamu alikuwa na uwezo wa kuwasiliana na kuongea na Mungu ana kwa Ana pasipo shida yoyote lakini uovu ulipoingia yale Mawasiliano yalikata gafla…
Mwanzo 3:6-10
[6]Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
[7]Wakafumbuliwa macho wote wawili wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo.
[8]Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.
[9]BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi?
[10]Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha.
Jiangalie sana ujihakiki katika wokovu wako ni wapi unalegalega upaimarishe,chunguza mwenendo wako wa uKristo,dhambi na mambo maovu ndiyo yanayofanya upoteze mawasiliano na mahusiano na Mungu,Acha uzinzi,ulevi,matukano na mambo yote mabaya ili uende sawa na Mungu…..
Shalom…
Amina
hakika
Ok
shalom
Wema wa Mungu
Uweza wa Bwana ni mkuu
Bwana Yesu asifiwe
Amen karibu..
Mungu ni mwema
mm
bwana ni bwana