Nakusalimu Kwa Jina Kuu la Mwokozi wetu Yesu Kristo,Jina litupasalo sisi kuokolewa kwalo….
Karibu katika muendelelezo wa kujifunza kwa njia ya Maswali na Majibu..”
●Swali
Naomba nifahamishwe hili,je tunapaswa kuishika sabato kwa namna gani?
●Jibu
Kabla ya kuanza kujua kuna umuhimu gani wa kuishika sabato au tunapaswa kuishika kwa namna gani ni heri ungejua kwanza nini maana ya sabato…
Sabato Kibiblia ni Pumziko, na Pumziko lenyewe linategemeana na Jambo lililofanyika mpaka ikapelekea kulifanyia Sabato jambo hilo….tukiingia Katika Biblia tunaona mpaka Mungu anajiwekea Sabato si kwa sababu ilizuka tu,si kwasababu anataka kupumzika bila Sababu,au alitaka na sisi tuwe na mapumziko”sivyo”….Biblia inasema….
Mwanzo 2:2-3
[2]Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.[3]Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Umeona hapo…Jambo lililompelekea Mungu kujitafutia sabato yake ni kwa sababu alifanya kazi sana katika kipindi kirefu,akaona si vema niendelee hivi kwa muda mwingi lazima nipate Pumziko kwanza..ndo hapo tunaona Bwana akatafuta siku yake akapumzika na Kustarehe…
Na ndivyo alivyofanya hata kwa taifa lake teule la Israeli kama tunavyosoma katika Maandiko… jinsi alivowatoa katika mikono ya watesi wao wamisri kwa mkono wake mkuu na wa ajabu,kwa ishara nyingi na miujiza tele,…
Kumbukumbu la Torati 5:6
[6]Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
Na lengo la Mungu kuwatoa huko si ili awape shida tena,si ili awasumbue Sumbue tena,si ili awatese na kuwaangamiza kwa mateso zaidi…Kwsababu Mungu baada ya mtu kufanya kazi nyingi anajua anahitaji Pumziko kwanza,anahitaji kustarehe kwa muda mwingi..ndivyo alivyowaona watu wake kwa kipindi kirefu cha utumwa na mateso na shida kwa masumbufu ya kila namna waliyopitia Israeli… huruma za Mungu zikashuka akaona sasa imetosha katika hayo, na sasa wanahitaji Pumziko lao…!!!
Kutoka 3:8
[8]nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Kumbe Kanaani ndio ilikuwa nchi yao ya mapumziko kwa Israeli yote baada ya utumwa na kufanya kazi kwa kipindi kirefu...Na ndo hapohapo Mungu anawapa Amri ya kuishika siku ya Sabato……tusome!!
Kumbukumbu la Torati 5:12
[12]Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru.
Umeona,,lakini ukiendelea kujifunza zaidi utagundua kuwa lengo la Mungu kuwaamuru Israeli kuishika sabato sio Waikariiri siku na tarehe na mwaka na kuiadhimisha kana kambwa iwe destruri kwao “ijapokuwa jambo hilo linaweza likawa jema sana mbele za Mungu,,,Lipo kusudi mpaka wanaamriwa kuishika sabato yao…Embu tusome kwa umakini….
Kumbukumbu la Torati 5:15
[15]Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
Umeona hapo eeh,,kumbe lengo kuu la wao kupewa sabato waishike sio kushika siku na kukumbuka tu kama siku nyingine zinazopita…Lengo ni wao WAKUMBUKE KWAMBA WAO WALIKUWA WATUMWA NA KWA UKUU WA MUNGU NDIO ULIOWATOA NA KUWAFANYA KUWA HURU TENA,hivyo wakae na kutafakari matendo makuu ya Mungu na kumtukuza na Kumshangilia kwa furaha na shangwe nyingi kwa kuwatoa katika mateso mengi…
Jambo hili bado linaendelea katika Agano letu hili jipya…
Yapo makundi ya wakristo bado wanaendelea kuidhamisha siku ya Sabato kwa kuishika na kufanya desturi…ndo mana Mtume Paulo kwa kulijua hilo akasema…
Wagalatia 4:9-10
[9]Bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?
[ 10]Mnashika siku, na miezi, na nyakati, na miaka.
Sisi wa Agano jipya tuna sabato yetu pia tuliyoamriwa tuishike Kama ndugu zetu wa Israeli walivyopewa….ndo mana wakati wanamshutumu Bwana Yesu kwa kuihalifu sabato na kutokuishika aliwajibu hapa…
Luka 6:5
[5]Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
Haleluya kwa Bwana,Kumbe Yesu Kristo ndiye sabato yetu,Yesu Kristo ndiye Pumziko letu…lakini Biblia ikaenda ndani zaidi kutuelezea kwa kina zaidi kwanini Yesu Kristo…embu tusome ….
1 Yohana 1:1-3
[1]Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kwa habari ya Neno la uzima;[2](na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena twashuhudia, na kuwahubiri ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
[3]hilo tuliloliona na kulisikia, twawahubiri na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
Yesu Kristo ndiye Neno la Mungu,Kumbe sabato yetu tunayopaswa kuishika na kuiadhimisha maishani mwetu ni Kuliishi na kulikumbuka kila wakati Neno la Mungu yaani Biblia takatifu….kwa namna yoyote na vyovyote vile hili ndo Pumziko letu kwa wanadamu wote…Biblia takatifu…..,
Hivyo kwa maarifa haya uliyoyapata katika Neno la Mungu,Yesu Kristo, yakupasa utoke huko katika destruri ambazo aziendani na Neno na kuanza Kumsikiliza Yesu Kristo katika Neno lake ili uonekane umeishika sabato kwelikweli…..
Bwana Yesu akubariki…
Washirikishe na wengine habari hizi njema…