Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo lihimidiwe milele na milele….
Nakukaribisha katika mwendelezo wa sehemu ya pili ya somo letu…Ni kwa Neema za Bwana hata imewezekana tena..
Leo kwa Baraka za Mungu tutaangazia tabia nyingine ambayo ukiwa nayo wewe mwanamke uliyeokoka basi inaweza ikaleta matunda mengi sana katika ufalme wa Mungu…na tabia hiyo si nyingine zaidi ya
●KUOMBEANA
Linawezekana likanonekana ni jambo dogo na la kawaida lakini likaleta matokeo makubwa sana katika kanisa…
Embu tujifunze kwa mfano wa kwenye Biblia ambao wote tunaufahamu lakini naamini siku ya leo lipo la kujifunza
Luka 2:36-37
[36]Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.[37]Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
Maandiko yanatuambia binti huyu na mama huyu ijapokuwa alipoteza mume katika usichana wake lakini aliona hakuna sababu tena za mimi kurudia kulekule tena…ni heri nitafute kilichobora zaidi ya nilichopoteza…na si kingine zaidi ya kuwa MWANAMKE MUOMBAJI….
Alifahamu nafasi kubwa na ya muhimu kwa mwanamke mcha Mungu ni pamoja na kuwa Mwobaji,, alifahamu kwa kuomba kwangu tu kunaweza kuleta matokeo mengi sana…ndo hapo tunaona kwa kitendo hicho tu Cha kujitoa kwa Bwana katika kuomba na kufunga na kudumu katika hekalu la Mungu akapewa ufunuo wa kujua Kristo yupo duniani…
Jiulize mwanamke uliyeokoka unadumu katika Maombi, unasimama kikamilifu katika kuombea Wanawake wenzako,kwenye kanisa ulilopo mna kikundi chenu cha maombi kila siku kwa ajili ya kuombeana, mna ushirika mmoja wa kubebana katika kuomba…
Maandiko yanasema
Yeremia 9:17-18
[17]BWANA wa majeshi asema hivi, Fikirini ninyi, mkawaite wanawake waombolezao, ili waje; mkatume na kuwaita wanawake wenye ustadi, ili waje;[18]na wafanye haraka na kutuombolezea, ili macho yetu yachuruzike machozi, na kope zetu zibubujike maji.
Biblia inamtaja mwanamke kama Mwombolezaji,,Na hii roho ipo kwa kila mwanamke(lazima ulifahamu hili)
Mwanamke unayo nafasi kubwa ya kusimama kuomba kwa ajili ya kanisa,taifa ,familia,injili na mambo mengi yanayohusiana na yakawa sawasawa na Kuomba kwako…
Anza kujizoesha sasa na ikawe ndo tabia yako ili uujenge Mwili wa Kristo….
Shalom…Washirikishe na wengine