Karibu tujifunze Maneno ya Mungu,Muumba mbingu na nchi,yeye aliyekuwepo tangu misingi ya ulimwengu hu haijawekwa 1 Petro 1:20
Ni neema za Bwana wetu Yesu Kristo kuiona siku nyingine ili tuweze kuongeza maarifa katika kumjua yeye milele yote…..
Maandiko yanatuambia tusiviangalie vinavyoonekana bali visivyoonekana, na leo tutavijua vinavyoonekana ni vipi na visivyoonekana ni vipi..
2 Wakorintho 4:18
[18]tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
Kiuhalisia yapo mambo ambayo hata sisi binadamu tukiyaangalia tunaona kabisa hayaendani na taswira ya kile tulichokuwa tunakitazamia,kwa macho yetu tunaweza kuona kitu kipo sawa au kitaleta matokea tuliyokuwa tunayaangalia lakini ikawa ndivyo sivyo…
Maandiko yanasema,.
Mithali 16:2
[2]Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;
Bali BWANA huzipima roho za watu.
Ndo hapo tunapokuja katika somo linalosema tusiviangalie vinavyoonekana bali visivyoonekana….yamkini yanayoonekana ni mazuri na yanavutia sana,kweli yapo mambo kwa taswira ya nje yanashawishika kwa kuonekana kwake tu lakini kiundani hayana matokeo yoyote mazuri
….Ndugu mpendwa,yakupasa uwe makini sana na mambo yote yanayokuja mbele yako au unayoyatazamia kuyafanya..kuwa macho na jambo lolote unalolitaraji mbele…vinavyoonekana katika hii dunia ni vingi sana,uzuri wake unapumbaza macho ya mwili hadi ya rohoni,
Kulipozuka ugomvi kati ya Lutu na Abramu iliwabidi kila mmoja kujichagulia mahali pa kwenda,maandiko yanasema lutu akainua macho yake akatazama na kuona sehemu yenye kuvutia yenye uzuri mithili ya Edeni
Mwanzo 13:10-11
[10]Lutu akainua macho yake, akaliona Bonde lote la Yordani, ya kwamba lote pia lina maji, kabla BWANA hajaharibu Sodoma na Gomora, lilikuwa kama bustani ya BWANA, kama nchi ya Misri hapo unapokwenda Soari.[11]Basi Lutu akajichagulia Bonde lote la Yordani; Lutu akasafiri kwenda upande wa mashariki; wakatengana wao kwa wao.
Laiti lutu angekaa na kuuchunguza na kutafuta kuyajua yale yaliyokuwa yanaendelea ndani ya ile miji,angepata kujua mazito yaliyokuwa ndani yake…lakini mwisho wake tunajua kama si huruma za Mungu lutu na familia yake wangeangamia katika ile miji..
Dada,Mama,Binti, urembo unaojiwekea katika mwili wako kwa nje unaonekana umependeza, unavutia, embu kaa chini uchunguze ndani ya hayo mapambo mwisho wake kuna hukumu gani,umekuwa ukisikia injili zinazokufurahisha tu moyo wako,kwamba njo kanisani utakavyo,njo ukiwa na suruali zako na vimini vyako njo ukiwa na wigi lako na utabarikiwa, ulishawahi kutulia na kuyachunguza maandiko jinsi wanawake wanavyopaswa kujisitiri…
Umekuwa mlevi wa kupindukia,unaiba wanaume za watu,matusi ni wewe,kejeli ni wewe,usengenyaji ni wako na mambo yote maovu ni yako,kweli kwa muonekano wa nje ni mambo yanayokupendeza,ni mambo yanayofurahisha moyo wako,unayafurahia sana lakini unafahamu mwisho wake ni nini,je hili andiko unalijua..
Warumi 6:23
[23]Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Embu itii injili ya Yesu Kristo inayokutoa kutoka umauti na kukuita uurithi uzima wa milele,embu anza kuvitafuta vile visivyoonekana kama mwandishi alivyotuhasa,akijua kabisa visivyoonekana ni Bora zaidi ya hivyo vinavyoonekana,
embu anza kuutafuta utakatifu,upendo wako uko wapi,utii, heshima na adabu,upole wako umeuweka wapi, haya na mengine mengi ni mambo yasiyoonekana lakini yakidhihirika kwa nje yatakuletea matokea makubwa na yenye thamani sana mbele za Mungu..
Kila siku kuwa mtu wa kuongeza maarifa kwa kusoma Neno la Mungu…….
Shalom..
Wasambazie wengine habari hizi njema
Amen ubarikiwe sana
Amina sana
Sifa na Utukufu Vyote ni Kwa Mungu pekee
Amina amina