Jina la mwokozi wetu Yesu Kristo litukuzwe milele…….
Karibu upate kujifunza kwa njia ya ndoto.
Asilimia kubwa ya ndoto tunazoota huwa zinatokana na shughuli nyingi tunazokutana nazo…mara nyingi ule mfumo unakuwa unajijirudia kwa njia ya ndoto…
Lakini kama umeona ndoto uliyoiota imekuja kwa uzito kidogo na haijaja kulingana na mizunguko yako mingi.. basi yakupasa uitafari kwa kutafuta maana yake mana hapo kuna jambo Bwana anatamani ulifahamu..
Biblia inasema..
Mhubiri 5:3
[3]Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.
Hivyo basi ukiota upo Jangwani peke yako au umeota upo katika jangwa mwenyewe na hakuna msaada wowote… ni ishara Yesu anakuonyesha jinsi gani ulivyomwacha Bwana na kuliweka tegemeo lako kwa vitu vya ulimwengu huu…yawezekawa ni wanadamu, mali, au wazazi….
Maandiko yanasema…
Yeremia 17:5-6
[5]BWANA asema hivi,
Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu,
Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake
Na moyoni mwake amemwacha BWANA.[6]Maana atakuwa kama fukara nyikani,
Hataona yatakapotokea mema;
Bali atakaa jangwani palipo ukame,
Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Jichunguze ni wapi umeweka tegemeo lako, jiangalie ni wapi umeweka tegemeo la maisha yako kwa wanadamu, wapi umeliweka tumaini lako mpaka umemsahau na kumwacha Bwana……
Jirekebishe na ugeuke kwa kutubu na kumrudia Bwana Yesu,awe mwokozi na tegemeo la maisha yako milele….
Bwana wetu anakuja…..